Jiji la Mwanza
Aidha,
watahiniwa wamefaulu zaidi somo la Kiswahili na kufeli zaidi somo la
Hisabati.
Katika
matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Baraza la Mitihani la Taifa
(NACTE), wavulana wameongoza somo la Hisabati kwa kupata alama 50/50,
ambapo 26 wamefaulu kwa kiwango hicho na wasichana wakiwa wanane.
Akitangaza
matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde, alizitaja
shule 10 bora kuwa ni Twibhoki ya Mara ambayo imeshika nafasi ya
kwanza, Mugini iliyoshika nafasi ya pili, Peace land na Alliance zote
za Mwanza, Kwema (Shinyanga), St. Severine (Kagera), Rocken Hill
(Shinyanga), Tusiime (Dar es Salaam), Imani (Kilimanjaro) na Palikas
(Shinyanga).
“Kwa
upande wa mikoa iliyofanya vizuri kitaifa na asilimia zake za ufaulu
kwenye mabano ni Dar es Salaam (46,434), Kilimanjaro (26,192), Mwanza
(37,017), Iringa (14,650), Arusha (23,250), Tanga (26,261), Njombe
(11,389), Kagera (24,501), Geita (17,560) na Mtwara (15,608).
“Wilaya
zilizoongoza kitaifa ni Mpanda Mji (Katavi), Biharamulo (Kagera),
Moshi (Kilimanjaro), Kibaha (Pwani), Arusha (Arusha), Kinondoni (Dar
es Salaam), Korogwe Vijijini (Tanga), Ilala (Dar es Salaam), Iringa
(Iringa) na Mji Makambako (Njombe),” alisema Dk. Msonde.
Akizungumzia
ufaulu wa kimasomo, alisema katika masomo yote umepanda kwa asilimia
kati ya 0.64 na 8.94 ikilinganishwa na mwaka jana.
“Watahiniwa
wamefaulu zaidi somo la Kiswahili ambapo ufaulu ni asilimia 69.70
tofauti na asilimia 69.06 ya mwaka jana, na somo walilofaulu kwa
kiwango cha chini zaidi ni Hisabati lenye ufaulu wa asilimia 37.56
ambapo mwaka jana ilikuwa ni asilimia 28.62.
“Katika
somo la Kiingereza watahiniwa waliofaulu kwa mwaka huu ni asilimia
38.84 ikilinganishwa na mwaka jana asilimia 35.52 na Sayansi kwa
mwaka huu waliofaulu ni asilimia 54.89 na mwaka jana asilimia 47.49,”
alisema.
Dk.
Msonde alisema jumla ya watahiniwa 451,392 kati ya 792,118 waliofanya
mtihani huo wamepata alama 100 au zaidi katika alama 250 ambapo idadi
hiyo ni sawa na asilimia 56.99.
Alisema
kati ya watahiniwa hao, wasichana ni 226,483 ambao ni sawa na
asilimia 53.59 na wavulana ni 224,909 sawa na asilimia 60.87.
Miongoni
mwa watahiniwa hao waliofaulu, Dk. Msonde alisema wamo wenye ulemavu
795 wakiwamo wasichana 355 ambao ni sawa na asilimia 44.65 na
wavulana 440 ambao ni sawa na asilimia 55.35.
“Katika
mtihani huo uliofanyika Septemba 10 na 11, mwaka huu jumla ya
watahiniwa 808,085 wa shule za msingi walisajiliwa kufanya mtihani
huo wakiwamo wasichana 429,624 sawa na asilimia 53.17 na wavulana
378,461 sawa na asilimia 46.83.
“Kati
ya watahiniwa hao waliosajiliwa, watahiniwa 691 walikuwa na uoni
hafifu, 87 walikuwa na ulemavu wa macho (wasioona), wenye matatizo ya
kusikia 374, wenye mtindio wa ubongo 252 na watahiniwa 27 walikuwa na
ulemavu zaidi ya mmoja,” alisema Dk. Msonde.
Pamoja
na mambo mengine, NECTA imemfutia matokeo mtahiniwa mmoja
aliyebainika kufanya udanganyifu katika mtihani huo. Mwaka jana
watahiniwa 13 walifutiwa matokeo yao kwa kufanya udanganyifu.
Hata
hivyo, Baraza hilo limesita kutoa matokeo ya shule zilizofanya vibaya
kwa madai ya kuendelea na uchambuzi wa kuzitambua zaidi.
0 comments:
Post a Comment