Monday 18 May 2015

Bingwa wa muziki wa Blues aaga dunia.


B.B. King - ambaye anatambuliwa kuwa bingwa wa muziki aina ya Blues ulimwenguni amefariki akiwa na miaka 89.
Jinsi anavyocheza gita lake kuliathiri pakubwa kizazi cha wacheza gitaa.
Alizaliwa Mississippi huko Marekani kulikokuwa na pamba na akafanya kazi katika mashamba akiwa bado mdogo.

Kisha aliajiriwa kama mwimbaji katika miaka ya arobaini kabla ya kuwa 'deejay' kabla ya kuanza muziki wake mwenyewe.
Alicheza katika hafla zilizovutia watu wengi akitumbuiza watu vizuri licha ya kuwa na umri wa miaka 80
Alisitisha ziara yake ya Marekani na Ulaya ili kuwatembelea wanawe 15.

Share:

Mgahawa wauza nyama ya binaadamu Nigeria.


Mgahawa mmoja nchini Nigeria katika jimbo la Anambra umefungwa kufuatia viongozi wenye mamlaka nchini humo kung’amua kwamba moja ya vyakula vinavyouzwa mgahawani humo ni nyama ya binaadamu.
Polisi walipoitwa mgahawani hapo waliona vichwa viwili vya binaadamu vipya vyenye kuchuruza damu wakati walipokuwa wakiwakamata watu kumi na mmoja kutoka mgahawani hapo akiwemo mmiliki wa mgahawa huo,pia walikamatwa wanawake sita na wanaume wane, baada ya wasamaria wema kutoa taarifa hizo za kustaajabisha!
Damu zilizokuwa zikivuja kwenye vichwa hivyo vya wanaadamu,vilikuwa vimefungwa kwenye mifuko ya Rambo.
Polisi pia wamekamata bunduki aina ya AK-47 na silaha nyinginezo,seti ya magurunedi na simu kadhaa za kila aina wakati walipokuwa wakiwakamata watu hao.
Kila wakati nilipokuwa nikienda sokoni,na sababu kubwa hasa hoteli hiyo iko karibu na sokoni,nimekuwa nikishuhudia harakati za ajabu za watu kuingia na kutoka hotelini humo,watu wachafu na uchafu wao mwilini ni ule usioeleweka,hivyo sikushangazwa polisi walipogundua biashara hiyo haramu mapema wiki hii, anasema mkaazi wa eneo hilo.
Mchungaji mmoja akiwa katika mshtuko mkubwa baada ya kugundua kuwa alikuwa amekula nyama ya binaadamu,aliamua kwenda polisi kupeleka malalamiko yake .
Aliwaambia kuwa alikwenda kwenye mgahawa wa hoteli hiyo asubuhi na mapema,baada ya kupata staftahi,akaambiwa kwamba pande la nyama alilokula gharama yake ni naira 700 sawa na paundi mbili unusu alistaajabu mno.sikufahamu kuwa nimeuziwa nyama ya binaadamu nikaila na kwamba ilikuwa ghali sana.
Taarifa za watu nchini Nigeria kula nyama za watu zimekuwa ni uvumi wa muda mreefu, lakini hii ni mara ya kwanza mgahawa kuamua kuuza nyama za binaadamu tu.
Share:

9 wauawa katika shambulio Marekani


Polisi nchini Marekani wamesema kuwa watu tisa wameuawa katika shambulio lililotekelezwa na watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki katika mkahawa mmoja katika mji wa Waco.
Hata hivyo watu wengine 18 walipelekwa hospitali kupatiwa matibabu kutokana shambulio hilo. Maofisa katika mji huo wanasema kuwa walibaini mkusanyiko kati ya watu watano walioonekana kupanga jambo lisilo la kawaida. Watu waliokuwa katika mkahawa huo walijificha katika chumba cha majokofu katika harakati za kujiokoa kabla ya kusaidiwa na Polisi kutoka katika eneo hilo.
Share:

Utafiti:Mazoezi yatakuongezea miaka 5 zaidi.


Utafiti umeonesha kuwa watu wanaofanya mazoezi ya kila mara wanaishi kwa miaka mitano zaidi ya wale ambao hawafanyi mazoezi yeyote.
Aidha utafiti huo uliowajumuisha watu waliokomaa umebaini kuwa watu walio na umri mkubwa wanaishi maisha marefu zaidi pindi wanaoacha kuvuta sigara.
Utafiti huo wa miaka 11 uliwajumuisha watu wazima 5,700 nchini Norway ulidhibitisha kuwa watu waliofanya mazoezi kwa takriban saa tatu kwa juma wanaishi zaidi ya miaka mitano zaidi ya wale ambao hawakufanya mazoezi yeyote.
Wanasayansi hao wameanzisha kampeini za uhamisisho wa faida za kufanya mazoezi hasa kwa watu wazima.

Wakiandika katika jarida moja la utabibu wa michezo linalochapishwa nchini Uingereza, wanasayansi hao wanasema kuwa maisha ya
kuketi bila ya kuwa shughuli yeyote inayochemsha damu mwilini inachangia pakubwa kuzorota kwa uwezo wa mwili kuhimili dhoruba ya maambukizo tofauti tofauti haswa mtu anapozeeka.
Chuo kikuu cha Oslo kilithibitisha kufuatia utafiti huo kuwa hata mtu akifanya mazoezi mepesi ni kheri kuliko kukosa mazoezi kabisa.
Takwimu za utafiti zinaonyesha kuwa japo watu wenye umri zaidi ya miaka 65 wakishiriki mazoezi yeyote kwa dakika 150, hiyo itatosha kumweka katika hali nzuri ya kiafya.

Aidha kwa wale wenye umri kati ya miaka 68 hadi 77 wanahitaji kufanya mazoezi kwa zaidi ya saa moja kwa juma ilikupata manufaa yake.
Kwa ujumla asilimia 40% ya washirika waliofanya mazoezi kwa takriban nusu saa kila siku walikuwa bado hai katika utafiti huo uliodumu kwa miaka 11.
Ripoti hiyo iliongezea kusema kuwa hata wale wazee waliokuwa na miaka 73 walipoanza mazoezi asilimia kubwa ilikuwa hai zaidi ya wenzao ambao hawakufanya mazoezi yeyote.
Share:

Indonesia yaombwa ikome kupima Ubikra..


Indonesia imeshauriwa ikomeshe sheria inayowalazimu wanawake kuthibitisha ni mabikira kabla ya kujiunga na jeshi la taifa.
Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wameihimiza serikali ya Indonesia kukomesha kipengee kimoja cha kubainisha iwapo mwanamke ni bikira au la kabla ya kujiunga na jeshi la taifa.
Wanaharakati hao wanasema kuwa ni tukio linalodhalilisha wanawake hao kwa misingi ya kijinsia.
Shirika la afya duniani WHO limepinga sheria hiyo likisema halina misingi yeyote kiafya.
Aidha shirika la Human Rights Watch (HRW) inaongezea kusema kwamba mtu kuwa au kutokuwa bikira hakuathiri utendakazi na uwajibikaji wa mwanamke kazini.
Lakini je nini kinachoendelea Indonesia?
Wanaharakati hao wanasema kuwa wengi wa makurutu ambao huwa ni wasichana waliohitimu shule ya upili wenye umri kati ya miaka 18-20
hulazimika kukaguliwa sehemu zao za uzazi ilikuthibitisha wangali ''wasafi na hivyo wazalendo''
Kulingana na shirika la kutetea haki za kibinadamu, sasa hata wachumba wa wanajeshi wao hawasazwi.

''wachumba wa wanamaji, wanajeshi wa angani na wanajeshi wa ardhini sasa wanalazimika kupimwa ubikira kabla ya kuruhusiwa kuolewa na maafisa''asema mwanaharakati mmoja.
Mwezi Februari maafisa wa jimbo la Jember ,Java Mashariki waliharamisha kujaribiwa kwa wasichana kabla ya kuhitimu shule za upili.
Je kipimo hicho kinafanywaje ?
Kulingana na mtafiti mmoja Andreas Harsono kipimo hicho kijulikanacho kama "two-finger test", kinatumika na madaktari kubaini iwapo mwanamke ni bikira au la.
Daktari anapaswa kung'amua iwapo mwanamke huyo ameshiriki tendo la ndoa au la.
''Daktari anatumbukiza vidole viwili ndani ya uke na kimoja katika tupu ya nyuma ''alisema mama mmoja mke wa mwanajeshi ambaye pia ni askari.
Bwana Harsono aliwahoji wanawake 11 wengi wao wake wa wanajeshi na wengine maafisa kivyao.
Hadi sasa haijabainika faida ya kipimo hicho ambacho kinalaumiwa kuwa kinawadhalilisha wanawake.
Amiri mkuu wa jeshi la Indonesia Meja Jenerali Fuad Basya,amesema kuwa kipimo hicho ni nguzo ya uzalendo na swala muhimu katika usalama wa taifa.
''Haiwezekani iwapo mtu ni msherati si muaminifu kwa mumewe apewe jukumu la kulinda usalama wa taifa''alisema Jenerali Fuad.
Kama mtu anapania kulinda mipaka ya taifa na pia usalama wa mamilioni ya watu ilihali ameshasaliti nafsi ya mumewe basi mtu kama huyo hapaswi kupewa jukumu la kulinda taifa''

''kama mwanamke si bikira iwe amegonjeka ama amejamiani hafai kuwa askari Hafai kuhudumu katika jeshi la Indonesia '' Jenerali Fuad alianukuliwa na vyombo vya habari.
Hata hivyo majibu yake yalitofautiana na ya mke mmoja wa mwanajeshi ambaye mwenyewe ni askari aliyesema kuwa walipewa sababu tofauti ya kipimo hicho.
''Wajua jeshi la Indonesia linataka wanajeshi wenye siha nzuri kwa hivyo wanalazimika kutumia mbinu kama hizo kupunguza gharama za matibabu ''
''Wanajeshi wetu wanasafiri kila baada ya muda na hivyo wanastahili kuamini kuwa wanawake wao na hata waume pia ni waaminifu''
Share:

Daktari wanaswa wakisinzia kazini




Je umewahi kushudia daktari akisinzia Hospitalini huku wagonjwa wakimsubiri ?
Katika mataifa mengi ya Afrika na Marekani Kusini ,kuna uhaba mkubwa wa madaktari jambo linalowalazimu madaktari na wauguzi wachache walioko kufanya kazi ya ziada ilikuwatuza wagonjwa.
Si ajabu kumsikia daktari anayehudumu katika hospitali ya umma ndiye yuleyule anayekimbia kumhudumia mgonjwa katika hospital ya kibinafsi iliapate pesa za ziada.
Je ni Uroho ama Uhaba wa madakari ?
Je mtizamo wako ni upi kinawapelekea madaktari hao kufanya kazi hata zaidi ya saa 8 zinazopendekezwa ?

Si Aghalabu visa vya madaktari kufanya makosa wakiwa katika vyumba vya upasuaji na hata mara nyengine katika vyumba vya wagonjwa mahututi kwa sababu ya uchovu.
Huko Mexico wagonjwa na jamaa zao wameanzisha kampeini ya kuwatetea wanafunzi wanaojifunza kazi.
Waliwapiga picha madaktari wakisinzia na kuzichapisha katika mitandao ya kijamii.
''inakuaje daktari ambaye anawajibu wa kuwatunza wagonjwa 12 anasinzia kazini''
''Hii ni kama rubani kusinzia ndege ikiwa angani ''anasema mwandishi wa blogu aliyechapisha picha hizo.

Watu waliochangia mjadala huo walidai kuwa madaktari wakuu wamekwenda kulala na kuwaachia wanafunzi wao kazi chungu nzima.
Baada ya mjadala huo katika vyombo vya habari ilibainika kuwa madaktari hao hufanya kazi wakati mwengine hata zaidi ya saa 36 bila mapumziko.
Wengi waliwashtumu madaktari waliohitimu wakisema kuwa wanawatelekeza wagonjwa wao kufuatia kuimarika maradufu kwa mishahara yao.
Share:

Wanajeshi washika doria Bujumbura


Jeshi nchini Burundi linapiga doria kwenye mitaa ya mji mkuu Bujumbura ambapo waandamanaji wameahidi kufanya maandamano ya kupinga uamuzi wa rais wa kuwania muhula wa tatu.
Wanajeshi wana matumaini ya kuwakamata wanajeshi waasi ambao waliongoza mapinduzi ya wiki hii katika jaribio la kumpindua rais Pierre Nkurunziza.
Nkurunziza ametaka kusitishwa kwa maandamano hayo na kuyahuzisha na jaribio hilo la mapinduzi.
Lakini baadhi ya makundi ya waandamanaji yamekana madai hayo na kumtaka tena rais kuiheshimu katiba.
Marekani nayo inasema kuwa Nkurunziza hastahili kuwania muhula mwingine ikiongeza kuwa serikali yake itawajibika kwa chochote kile kitakachotokea.
Share:

Rais Mutharika amlilia mwandishi wa BBC


Rais Peter Mutharika wa Malawi ametoa salaam za rambirambi kufuatia kifo cha mwandishi wa habari wa BBC nchini humo Raphael Tenthani, ambaye amekufa katika ajali ya gari.
Bwana Mutharika amesema, Tenthani atakumbukwa kama mtu mwenye kipaji cha hali ya juu, mcheshi na mchangamfu.
Raphael Tenthani ambaye alikuwa na umri wa miaka 43 alifahamika nchini kote Malawi na amekuwa akiripotia Idhaa ya Kiingereza ya BBC kwa zaidi ya miaka kumi. Pia alifanya kazi na shirika la habari la Marekani la Associated Press. Mwaka 2010 alishinda tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Vyombo vya Habari kwa kazi yake kuhusu Malengo ya Maendeleo ya Milenia.
Share:

Mashua za wahamiaji kuharibiwa


Mawaziri wa nchi za muungano wa Ulaya wanakutana leo kuidhinisha mipango ya kuharibu mashua zinazotumiwa kusafirisha wahamiaji kwenda Ulaya kutoka nchini Libya.
Mara mipango hiyo itakapothibitishwa ujumbe wa muungano wa Ulaya utakusanya habari kuhusu shughuli za walanguzi wa binadamu na kulenga mashua zao baharini.
Viongozi wa Ulaya wanalenga kuchukua hatua kama hizo za kijeshi eneo la bahari la Libya na pwani ya Libya.
Karibu wahamiaji 6000 wanakadiriwa kuvuka bahari kutoka Afrika kaskazini na kuingia Ulaya mwaka huu.
Share:

Wavuvi waagizwa kutowasaidia wahamiaji


Wavuvi kutoka Indonesia wamesema kuwa wameamriwa na Serikali kuwa wasiwalete wahamiaji wanaopatikana wakielea kwenye vyombo baharini wasiokuwa na chakula au maji ya kutosha.
Maelfu ya wahamiaji wanadhaniwa kuwa wanaelea Baharini katika maeneo karibu na Indonesia, Thailand na Malaysia.

Licha ya wito wa Umoja wa Mataifa kuwa wahamiaji waruhusiwe kufika ufuoni, mataifa hayo matatu yamefukuza boti zilizojaa wahamiaji.
Ni wale watu wanaojitahidi kufika nchi kavu pekee wanaoruhusiwa katika nchi hizo.

Wahamiaji wengi ni Waislamu wa jamii ya Rohingya wanaotoroka mateso nchini Mynamar.
Watu wengi wanataka taifa la Myanmar kuchukua wajibu mkubwa zaidi kuhusiana na wahamiaji hao lakini taifa hilo limekataa likidai kuwa halipaswi kulaumiwa kwa hali hiyo.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.