Tuesday 18 November 2014

AJILIPUA KWA MAFUTA YA TAA..........source Global Publisher


Kijana mmoja Nicholas Mhagama (25), mkazi wa Makongo Juu Dar,  juzi kati alijilipua na mafuta ya taa kisa kikidaiwa kunyanyaswa na babu yake. Tukio hilo lilitokea eneo la Makongo Juu Makaburini usiku ambapo kijana huyo na babu yake aliyemtaja kwa jina moja la Mhagama waligombana.


 Kijana Nicholas Mhagama (25) aliyejilipuwa na mafuta ya taa akidai kunyanyaswa.
Share:

Netanyahu aishutumu Palestina na Hamas........sourse BBC



Benjamin Netanyahu

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amewataka Waisrael kuungana bila kujichukulia sheria mkononi baada ya Wapalestina wawili wakiwa na bunduki na mashoka kuwaua waumini wanne katika hekalu moja mjini Jerusalem.
Ameyashutumu Mamlaka ya Palestina na Hamas kwa kuchochea shambulio hilo. Lakini maafisa wa Palestina wamemlaumu Netanyahu kwa kuchochea ghasia kubwa za hivi karibuni, zilizosababisha Waisrael na Wapalestina kuuawa.
Amesema kama taifa watakabiliana na ugaidi na wafadhili wao.Hata hivyo Netanyahu ameongeza kuwa kwa sasa wapo katika kampeni ndefu ya vita dhidi ya ugaidi na ambayo haikuanza leo.
Netanyahu amesisitiza kuwa kuna watu baadhi ya watu wanaotaka kuwandoa katika mji mkuu wa Israel Jerusalem, suala ambalo amesema haliwezekani kwani huo ni mji mkuu wao milele
Share:

Bi harusi apewa talaka siku ya harusi..... source BBC



Bi harusi apewa talaka siku ya harusi.Picha niaba ya gazeti la Daily Mirror nchini Uingereza 

Bwana harusi mmoja kutoka Saudi Arabia amempa talaka mkewe siku ya harusi baada ya kumuona uso wake kwa mara ya kwanza wakati mpiga picha alipotaka kuwapiga picha.
Maharusi hao kutoka mji wa magharibi wa Saudia,Medinah walikubaliana kuoana licha ya kutoonana uso kwa uso,swala ambalo ni utamaduni mkubwa wa mataifa ya mashariki ya kati.
Lakini wakati mwanamke huyo alipofungua kitambara alichokuwa amejifunika uso na kutabasamu katika kamera,mumewe alishtuka na kuondoka wa ghafla.
Kulingana na gazeti moja katika eneo hilo kwa jina Okaz,mwanamume huyo alianguka na kuzirai huku wageni waalikwa wakijaribu kuingilia kati ili kutatua kilichokuwa kikiendelea.
Hata hivyo Bwana harusi alisema kuwa hakuweza kumwona bi harusi kabla ya harusi yao gazeti hilo la Okaz liliripoti.
'' Si wewe msichana niliyetaka kuoa,si wewe kamwe niliyedhani '' kwa hivyo nakupa talaka''alisema bwana harusi.
Na alipompa talaka bi harusi naye alianguka na kuzirai na kuifanya harusi hiyo kuwa usiku wa majonzi.
Share:

Shahidi mkuu kuhusu Rwanda atoweka Kenya


Kumbu kumbu ya mauaji ya Kimbari nchini Rwanda

Shahidi mmoja muhimu wa uchunguzi unaofanyika kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda ambaye alikuwa akitarajiwa kuhojiwa na majaji Nchini Ufaransa kuhusu kudunguliwa kwa ndege ya aliyekuwa rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana, anasemekana kutekwa nyara na kutoweka jijini Nairobi.
Idara ya Polisi Nchini Kenya imekanusha kumtia mbaroni Emile Gafirita.
Majirani wa Emile Gafirita wanasema kuwa walisikia milio ya breki za gari na kamsa pale alipokuwa akirejea nyumbani muda mfupi kabla ya usiku wa manane Jumatatu usiku na kuwaona watu wawili wakimtia pingu na kumrusha kwenye gari.
Idara ya Polisi Nchini Kenya inasema kuwa hawajamtia mbaroni.
Jina la bwana Gafirita liliibuka katika kesi ya hivi majuzi Nchini Rwada, pale alipotajwa kama askari wa zamani katika kikosi cha ulinzi cha Rais Paul Kagame.
Majaji wawili wa Ufaransa, Marc Trevidic na Nathalie Poux, walikuwa wakipanga kumhoji ili atoe ushahidi mjini Paris kuhusiana na mzinga ulioshambulia na hatimaye kuiangusha ndege iliyombeba Rais wa zamani wa Rwanda hayati Juvenal Habyarimana mnamo mwezi Aprili ya mwaka 1994.
Mauaji ya Habyarimana yaliibua mapigano makali ya kikabila yaliyosababisha mauwaji ya zaidi ya watu laki nane, wengi wao waTusti na wahutu wenye siasa za kadri.
Share:

15 wakamatwa kwa mauaji Mombasa


Polisi mjini Mombasa wamewakamata watu 15 kuhusiana na mauaji ya watu wanne usiku wa kuamkia leo mjini humo.
Lakini wamekanusha kuwa mauaji hayo yalihusishwa na msako wa polisi dhidi ya misikiti inayotoa mafunzo ya itikadi kali mjini humo.
Hali ya taharuki bado iko juu katika baadhi ya maeneo mjini humo huku polisi wakiendelea kushika doria mjini humo.
Kamishna mkuu wa Mombasa, Nelson Marwa anasema kuwa wale wote waliohusishwa na mauaji hayo ya watu wanne kwa kuwadunga visu, walikodiwa na mwanasiasa katika mtaa wa Kisauni.
Marwa hata hivyo amesema idadi ya wale waliouawa sio watu wanne bali ni watatu.
Hata hivyo jamaa wa waliouawa walithibitisha idadi yao kuwa watu wanne ambao walifariki baada ya kudungwa visu.
Wengine zaidi ya 12 walijeruhiwa kwenye tukio hilo ambalo limejhusishwa na vijana wenye itikadi kali za kidini.
Zaidi ya vijana 250 walikamatwa baada ya kupatikana na maguruneti pamoja na silaha nyinginezo kwenye msako uliofanywa Jumatatu asubuhi.
Viongozi wa kiisilamu na mashirika mengine ya kutetea haki za binadamu wamelaani msako huo ambao wanasema utarejesha tu hisia za waisilamu kulengwa na maafisa usalama.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.