Kundi
la Al Shabaab nchini Somali linasema kuwa limefanya mashambulizi ya
abiria 28 katika basi moja kazkazini mashariki mwa kenya.
Basi
hilo ambalo lilikuwa likiwabeba abiria 60 lilitekwa katika jimbo la
mandera lilipokuwa likelekea mjini Nairobi.
Abiria
mmoja ambaye alinusurika ameiambia BBC vile raia wasio wa Somali
walitengwa na wengine na wale ambao hawakuweza kusoma aya ya Quran
walipigwa risasi kwa karibu.
Katika
taarifa yake al Shabaab limesema kuwa mashambulizi hayo ni ya
kulipiza kisasi mauaji ya waislamu huko Mombasa yaliotekelezwa na
vikosi vya usalama vya kenya.
Kenya
imekumbwa na misururu ya mashambulizi ya risasi na mabomu yanayodaiwa
kutekelezwa na kundi la Alshabaa tangu vikosi vyake viingie nchini
Somali
0 comments:
Post a Comment