Friday, 28 November 2014

Mtoto mchanga anusurika kuuawa Kenya.....


Mtoto X amelala kwa utulivu, akiwa amefunikwa na Blanketi lenye kumpa joto na kukumbatiwa na Mama yake katika Nyumba moja ya kulelea Watoto yatima nchini Kenya.
Mtoto huyu ni wa miezi miwili hivi sasa, alizaliwa kufuatia tendo la ngono kati ya msichana na Mjomba wake, mtoto huyu anaelezwa kupatikana katika mazingira ya miiko.
Katika nyumba ya watoto wa Kanduyi, mjini Bungoma magharibi mwa Mji wa Nairobi, kama ilivyo kwa Watoto wengine , Mtoto huyu aliokolewa kutoka kwenye Familia yake kulipokua na mipango ya kuuawa.
Katika tukio hilo,siku mbili tu baada ya kuzaliwa Mtoto X, baada ya kupewa Taarifa vikosi vya usalama vilivamia makazi ya mtoto huyo na kumchukua wakiyaokoa maisha yake kutokana na kifo kilichokuwa kinamkabili mbele yake, kifo kilichaoamriwa na wazee wa kimila wa jamii iitwayo Bukusu.
Kuna watoto kama yeye katika nyumba hii ya Kunduyi wenye umri kati ya siku moja mpaka miaka 18.
Watoto waitwao 'mwiko'
Kujamiiana kwa maharimu ni mwiko nchini Kenya kama ilivyo katika maeneo mbalimbali, kwa mujibu wa Sheria ya Kenya, hilo ni kosa lenye kuadhibu kwa kifungo cha miaka mitano,au kifungo cha maisha kwa kujamiiana na binti wa umri mdogo

Lakini kwa Karne nyingi, adhabu ya kimila katika Jamii nyingi za Kenya ni kifo,na katika jamii ya Bukusu si lazima Mwanaume na Mwanamke waliohusika, lakini pia mtoto atakayezaliwa kutokana na uhusiano ulio mwiko.









Waziri wa utamaduni katika Kaunti ya Bungoma,Stephen Kokonya amesema kumekuwa na mahusiano ya namna hii yameenea katika jamii na kuongeza kuwa si sheria kwa jamii kutoa adhabu ya kifo, ni Jaji pekee anayeweza kuhukumu.Kokonya amesema katika maeneo ya kijijini hii ni sehemu ya Sheria za kijamii watoto kuonekana kuwa wamelaaniwa.
Watu wa jamii ya Bukusu huwaita Watoto hawa ''be luswa'' wakimaanisha ''Watoto haram'' wakihofu kuwa watasababisha kupata laana kama utasa na magonjwa ya akili.
''Kila mara tunaposikia mtoto anayedaiwa kuwa haramu amezaliwa katika eneo lolote huwa tunakimbia upesi kumuokoa vinginevyo unaweza kufika na kuambiwa tayari Mtoto alishakufa''Afisa anayetunza Watoto katika nyumba ya Watoto wa Kanduyi,Alice Komotho ameiambia BBC.
Kokonya amesema Serikali inatoa elimu ya uelewa kuhusu vitendo vya adhabu zitolewazo kinyume cha sheria ya nchi na Wazee wa jamii ya Bukusu.
Kisa cha Msichana.
Mama wa miaka 15 ambaye mtoto wake aliokolewa amerudi shuleni,binti huyu wa miaka 15 alibakwa na Mjomba wake. Msichana huyu amesema Mjomba wake alimtishia kuwa atampiga ikiwa atatoa taarifa kuhusu tukio la kubakwa, binti huyu alibakwa na mjomba wake mwenye umri wa miaka 17.
Msichana huyu hivi sasa amerudi shuleni kurudia mwaka wake alioupoteza alipokua mjamzito.
Binti huyu anaeleza kuwa hana mapenzi na Mjomba wake wala mtoto wao.
Mama huyu mdogo ameiambia BBC kuwa anapenda kuwa Daktari atakapomaliza masomo.
Maafisa wanasema kuwafundisha wazee wa kimila itakua ni njia nzuri ya kumaliza mila na desturi mbaya katika maeneo ya vijijini.
Mjomba wa Msichana huyo alikataa kuzungumza na BBC baada ya kuwasiliana nae.
Haki ya Kuishi
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wazee wa Bukusu anaeleza namna mtoto anavyouwawa,anakataa kuzungumzia kisa cha Mtoto X lakini anaeleza namna mtoto wanayedai kuwa haramu anavyouawa, anaeleza..
''Wakati binti anapokaribia kujifungua,huwakusanya baadhi ya Wanawake ambao hujifanya kama wanakwenda kumsaidia mzazi badala yake humziba pumzi mtoto kwa kuzibana nyonga za mama na kumuua Mtoto.
Wakinamama hawa hufanya haya kwa makini wakiamini kuwa ni budi mtoto kufa ili mzazi aishi katika jamii kwa amani.
Mzee mwingine anasema pia Wanakijiji wakati mwingine huua uzao wa pili ambao huwa pacha kwa madai kuwa huleta hali ya bahati mbaya, ambao wanapenda kubaki na watoto wao hulazimishwa kuondoka kijijini hapo.
Lakini Waziri wa utamaduni anasema kuwa angependa kuwakumbusha Wazee wote ambao hukaa na kuamua maamuzi ya mauaji kuwa wanaingilia haki ya msingi ya kuishi.
Share:

0 comments:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.