Taarifa kutoka mjini Kano, Kaskazini ya Nigeria, zinasema kuwa watu wengi wamefariki na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulizi la bomu.
Ni
baada ya milipuko mitatu inayoaminika kuwa ya mabomu kutokea katika
msikiti mkubwa zaidi mjini humoulio katikati mwa jiji karibu na eneo
anakoishi Emir au kiongozi wa waisilamu nchini humo Muhammad Sanusi.
Emir
huyo kwa sasa yuko nchini Saudi Arabia.
Mabomu
hayo yalilipuka wakati maombi ya Ijumaa yalipokuwa yanaendelea.
Mtu
mmoja aliyeshuhudia tukio hilo, alihesabu karibu miili 50 ya
waliofariki katika shambulizi hilo.
Taarifa
zingine zinasema watu waliokuwa wamjihami waliaingia msikitini humo
na kuanza kufyatua risasi baada ya mabomu kulipuka.
Wapiganaji
wa Boko Haram, wamekuwa wakifanya mashambulizi katika mji huo ambao
ni mkubwa zaidi Kaskazini ya Nigeria.
Mapema
mwezi huu , Emir alitoa wito kwa watu kujikinga dhidi ya mashambulizi
yanayofanywa na Boko Haram.
Aliwashauri
wakazi kujihami na kufanya kila wawezalo kujikinga dhidi ya
mashambulizi yanayofanywa na kundi hilo.
Msemaji
wa Polisi alisema matamshi ya Emir, yalikuwa ya uchochezi na kwamba
watu wanapaswa kumpuuza.
0 comments:
Post a Comment