Menu - Pages

Thursday, 26 February 2015

BBC yawateua Vijana wabunifu Kenya..


Makundi mawili ya ubunifu wa kiteknoligia wameteuliwa kuisaidia shirika la utangazaji la BBC kuafikia ruwaza yake ya kupanua upeo wa usikilizaji wa vijana kupitia kwa mfumo mpya wa kidijitali.
Vijana hao wataalamu wa digitali kutoka muungano wa Go Sheng na Ongair walichaguliwa kutoka timu 13,zilizoshiriki mashindano hayo kutoka Afrika na Marekani.
Mashindano ya ubunifu "hackathon" ya BBC yalilofanyika mjini Nairobi Kenya mapema mwezi huu.
Watafadhiliwa kufanikisha majaribio ya miundo msingi waliozindua kwa kipindi cha miezi sita ijayo.
‘’Nimefurahia kwamba studio ya kwanza iliyoshikanishwa ya BBC Afrika inalengo la kuchochea vipaji vya ubunifu hapa hapa barani'' alisema
Dmitry Shishkin mhariri wa BBC wa maswala ya kiteknolojia ya dijitali.
Bwana Shishkin alikuwa miongini mwa wakaguzi katika mashindano hayo ya ubunifu.
Timu mbili zilizochaguliwa zilikuwa zimepeana natharia mahsusi ya jinsi ya kuwafikia vijana kupitia mfumo huu wa kidijitali.
Kundi la Go Sheng lilipendekeza kuwafikia wasilikizaji na watazamaji wa BBC kupitia lugha ya mtaani iitwayo ''Sheng''
Nahodha wa kundi hilo Euticus Mola alisema kuwa wanatazamia kuwafikia vijana kupitia kwa lugha ya sheng.
Aidha wapinzani wao Ongair nao walipendekeza kufungua njia za mawasiliano na vijana kwa nia ya kuwakutanisha vijana na kuelewa matakwa yao.
Kiongozi wa kundi hilo Trevor Kimenye 30 aliiambia BBC kuwa mbinu hiyo anahakika itawezesha vijana kujieleza.

No comments:

Post a Comment