Menu - Pages
▼
Monday, 8 June 2015
Jeshi la Nigeria lahamia Maiduguri
Makao makuu ya jeshi la kulinda usalama la Nigeria limehamisha kitovu cha operesheni ya kukabiliana na wapiganaji wa kundi la kiislamu la Boko Haram hadi mji wa Maiduguri.
Hatua hii inafuatia ahadi ya rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari alipokuwa akiapishwa kuwa moja ya kauli mbiu ya utawala wake ni kukabiliana na Boko Haram.
Msemaji wa jeshi kanali Sani Usman amesema kuwa wanajeshi wakuu wote wamehamia huko ilikuendesha operesheni dhidi ya kundi hilo.
Mji huo ulioko kaskazini mwa taifa hilo tajiri zaidi barani Afrika kiuchumi umekuwa kitovu cha mapigano makali baina ya wapiganaji wa Boko haram na majeshi ya serikali.
Katika siku za hivi punde Maiduguri Imeshuhudia visa vingi mno vya mashambulizi ya kujitolea mhanga ambayo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 80.
Rais mpya aliyechaguliwa majuzi, Muhammadu Buhari, aliamuru kuhamishwa kwa kituo hicho hadi Maiduguri kutoka mji mkuu wa Abuja - mahala ambapo aliapishiwa mwishoni mwa mwezi uliopita.
Mwana habari wa BBC wa maswala ya usalama barani Afrika, amesema kuwa kumekuweko na lawama dhidi ya makamanda wakuu wa kijeshi kujitenga na hali ilivyo katika kikosi cha kwanza kinachopambana na Boko Haram.
Hali hiyo imechangia pakubwa kutokuwa na uwezo wa kufanya maamuzi ya busara.
Amesema kuwa uamuzi huo wa kuhamishiwa kwa kituo hicho kikuu hadi Maiduguri, kutasaidia pakubwa katika vita dhidi ya Boko Haram, kundi ambalo limesababisha maafa makubwa na hasara Nchini Nigeria.
No comments:
Post a Comment