Menu - Pages
▼
Wednesday, 15 July 2015
Mahujaji 27 waaga dunia India
Zaidi ya mahujaji 27 wameuawa kufuatia mkurupuko uliotokea katika warsha moja ya kidini katika jimbo la Andhra Pradesh nchini India.
Mkanyagano huo ulitokea wakati wa kuanza kwa sherehe za Maha Pushkaralu ambapo maelfu ya watu waliokuwa wamekusanyika kuoga kwenye maji ya mto Godavari walianza kusukumana.
Mkurupuko huo ulitokea mwendo wa saa nane u nusu katika mji wa Rajahmundry
Polisi wanasema kuwa umati ulikimbia kwenda kwa lango la kuinga mtoni.
Mikurupuko kama hii hutokea kwa wingi wakati wa warsha za kidini nchini India ambapo watu wengi hung'ang'ania nafasi katika maeneo madogo.
Waandalizi wanasema kuwa takriban watu milioni 24 wanatarajia kushiriki katika hafla hiyo inayotarajiwa kudumu kwa siku 12.
Mahujaji hao wa dini hiyo wanaamini kuwa kuoga na maji ya mto huo huosha mtu madhambi yake.
Waziri mkuu wa jimbo hilo Andhra Pradesh bwana Chandrababu Naidu, alisema kuwa inahuzunisha mno kuwa mahujaji waliokuwa wakitarajia kuosha madhambi yao wanaangamia.
Mwaka wa 2013 watu 115 walipoteza maisha yao katika mkurupuko uliotokea katika hafla ya kidini ya wahindu katika jimbo la Madhya Pradesh
No comments:
Post a Comment