Menu - Pages
▼
Monday, 20 July 2015
Rais wa zamani Chad,ashtakiwa Senegal.
Rais wa zamani wa Chad Hissene Habre atafikishwa mahakamani nchini Senegal kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu, ukatili dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita .
Kesi hiyo mjini Dakar ni ya kwanza ya aina yake ambapo nchi moja ya Afrika imemshitaki kiongozi wa zamani wa taifa jingine.
Bwana Habre anashutumiwa kwa kuhusika na vitedo vya ukatili na mauaji ya maelfu ya watu wakati wa enzi ya utawala wake kuanzia 1982 hadi 1990, shutuma anazozikanusha..
Kesi hiyo inafuatia miaka 25 ya kampeni za kumfikisha mbele ya sheria.
Wengi miongoni mwa watu wanaodaiwa kuwa waathirika wa uhalifu uliotekelezwa na Bwana Habre' wamekua wakitoa wito wa kufunguliwa mashtaka dhidi yake tangu alipopinduliwa mamlakani na kukimbilia uhamisho nchini Senegal 1990.
Mnamo mwaka 2005 mahakama ya Ubelgiji iliytoa kibali cha kumkamata, ikidai kuwa na haki ya kimataifa ya kufanya hivyo , lakini baada ya mazungumzo na Umoja wa Afrika , AU iliiomba Senegal kuendesha kesi dhidi Bwana Habre " kwa niaba ya Afrika ".
No comments:
Post a Comment