Menu - Pages
▼
Monday, 16 February 2015
Waliowajeruhi polisi TZ wasakwa........
Polisi nchini Tanzania wamesema wanawasaka watuhumiwa waliowajeruhi askari sita kwa risasi mkoani Tanga.
Askari hao walijeruhiwa wakati wakifanya kazi ya kuwatafuta watuhumiwa wa uhalifu wa kutumia silaha wanaodaiwa kuwa walijificha eneo moja nje ya mji wa Tanga wakiwa na silaha.
Awali kulizagaa taarifa na hofu kuwa wahusika walikuwa na itikadi za kigaidi, lakini taarifa ya maandishi iliyotolewa na polisi imewaita watu hao kuwa ni majambazi na kwamba msako wa kuwatafuta unaendelea.
Hata hivyo taarifa haikuleleza wanaotafutwa ni watu wangapi, ingawa imetaja kuhusika kwa jeshi lenye silaha jambo linaloashiria mapambano yalikuwa makali.
Oscar Pistorius apandishwa hadhi jela....
Kuhusiana na mwanariadha Oscar Pistorius aliyeko kifungoni, imeelezwa kwamba sasa anaweza ama kuruhusiwa kukumbatiana na wageni wake na hata kuwabusu wanaomtembelea ,anaruhusiwa kusikiliza redio na hata kuvaa vitu vya thamani ikiwemo vito vya thamani akiwa ndani ya gereza.
Mtuhumiwa huyo wa mauaji,amepewa ruhusa ingine ya kuwa huru kupiga simu atakavyo,vile vile bajeti yake inayodaiwa kuwa kubwa, imekubaliwa aweze kununua vyoo atakavyo na hata akitaka chipsi ataletewa,na huu ni uamuzi wa bwana jela anaye angalia wafungwa na hadhi zao naye Pistorius yuko kundi B.
Ikumbukwe kwamba Oscar alimuua mpenzi wake mnamo mwezi kama huu na siku inayotajwa kuwa muhimu ulimwenguni tarehe ya kumi na nne Valentine's Day,mwaka wa jana akiwa nyumbani kwake.
Akiwa jela Pistorius anajaribu kuyazoea mazingira ya jela na inamuwia vigumu kukubali kuwa ameupoteza uhuru wake, na pia kuonekana kama tishio la usalama na hivyo yumo ndani
Msemaji wa familia ya Pistorius mwanamama,Annalise Burgess, amemzungumzia mwanariadha huyo aliyekuwa maarufu duniani kiasi cha kupachikwa jina la Blade Runner,sasa amepandishwa hadhi na kuwa daraja la A .
Familia ya Oscar ina Whatsapp la familia yao ambalo linafuatilia taarifa zote za mwanariadha huyo na pia hutumia akaunti hiyo kujadiliana masuala ya biashara za familia.
Inaelezwa kuwa watu wanaoongoza kumtembelea Oscar Pistorius Jela ni kaka na dadake Aimee Carl na wakiisha kuonana naye hutuma taarifa na picha katika kundi hilo na kinachoendelea kumhusu yeye gerezani.
Kupandishwa kwa Oscar kuna maanisha kuwa anaruhusiwa kutembelewa na wageni zaidi ikiwemo familia yake.Hapo mwanzo kila anayemtembelea huzungumza naye kwa njia ya simu akiwa ametengwa na mgeni wake na vioo, na hakuruhusiwi kuguswa,lakini mambo sasa yamebadilika.
Sasa Oscar mwenye umri wa miaka ishirini na nane, anaweza kuwakumbatia jamaa zake wamtembeleapo,na muda wa kumuona umeongezwa kutoka saa mbili hadi tatu kwa mwezi,na wageni wamtembeleao bado wanakabiliwa na sheria ya kupekuliwa kabla ya kuonana ma mfungwa huyo ambaye bado anatakiwa kuvaa sare za jela zenye rangi ya samawati ama ita orange
Suala la hadhi ya Oscar kupandishwa daraja limewakera wafungwa wenziwe walioko kwenye gereza la Death Island: lilotengwa,ambalo limezunguukwa nyaya za umeme wamelalama kuwa mwanariadha huyo mlemavu anapewa hadhi ya kifalme kwa muda mfupi sana ilhali wao wanataabika muda mrefu gerezani.
Runinga 3 Kenya zimezima matangazo yao..
Kampuni tatu kubwa za kibinafasi za utangazaji zimesitisha kupeperusha matangazo kwenye televisheni kwa muda wa siku tatu zilizopita,
baada ya serikali kudhibiti mitambo ya zamani ya kupeperusha matangazo kwa mfumo wa analojia.
Kampuni hizo za Standard Media, inayomiliki runinga ya kwanza ya kibinafsi nchini Kenya KTN Nation media Group inayomiliki NTV na QTV
na Royal Media Services inayomiliki Citizen TV zimekuwa katika malumbano makali na serikali kuhusu uhamiaji wa kupeperusha matangazo kwa kutumia mfumo wa digitali kutoka ule wa zamani analojia.
Runinga hizo tatu zimekuwa zikilumbana na halmashauri ya serikali ya mawasiliano kuhusu swala la kuhama kutoka mfumo wa zamani hadi digitali kwa zaidi ya miaka nne sasa.
Hatua ya mwsihoni mwa wiki ya kufunga mitambo ya zamani ya kurushia matangazo yaani analogue ya runinga hizo ilichukuliwa baada ya amri ya mahakam ya juu zaidi nchini Kenya kuidhinisha uhamiaji huo.
Wamiliki wa runinga hizo tatu wanasema hawajajiandaa vilivyo kwa uhamiaji huo.
Lakini, je, nini hasa chimbuko la vyombo hivyo tatu vya habari kusitasita katika uhamiaji huu wa digitali?
Mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa vyombo vya habari vya Kenya anasema kuwa Serikali ilipendelea vyombo vya habari vinavyomilikiwa na wageni na hivyo kuwanyima fursa wakenya kumiliki na kuchangia katika ukuaji wa
sekta ya utangazaji nchini Kenya.
Kwa sasa, watazamji wanategemea sana vituo viwili vikubwa, kile cha K24 ambacho kinadaiwa kumilikiwa na familia ya rais wa Kenya na runinga ya kitaifa ya shirika la utangazaji la Kenya.
Kwa upande wake, serikali ya Kenya kupitia halmashauri ya mawasiliano CAK inasisistiza kwamba zaidi ya wakenya asilimia 60 wanavyovijisanduku vipya vya kuwawezesha kupokea matangazo kwa njia ya digitali.
Katika mitaa ya mji mkuu wa Nairobi, baadhi ya wakenya wanaelezea jinsi walivyokosa kutizama vipindi vyao wanavyovipenda.
Hata hivyo wengine wanakubaliana na serikali kuwa sharti mipango ya serikali ya kuhamishwa kwenye masafa ya kidijitali yaendelee mbele ilikufungua sekta nzima ya sanaa.
Kulingana na sera za serikali ya Kenya runinga zote zinahitajika kuandaa na kupeperusha asilimia 60% ya vipindi kutoka nchini Kenya huku asilimia 40 ikiwa vipindi kutoka ughaibuni.
Wakenya wengi wanahisi kuwa serikali iliharakisha uhamiaji huo ila wangependa sekta nzima ifuate sheria za nchi.
Mnano mwaka wa 2006, kongamano la kimataifa kuhusu mawasiliano lililoandaliwa mjini Geneva Switzerland liliazimia kwamba nchi wanachama ziwe zimehama kutoka mfumo wa zamani wa utangazaji wa analogue hadi digitali
ifikapo tarehe 17 mwezi juni mwaka wa 2015.
Ingawa tarehe hiyo bado haijawadia, mamilioni ya watazamji wanaotegemea runinga za KTN, NTV na Citizen tayari wanaonja athari za kukera za maendelezi ya teknologia.
Misri yaishambulia ISIS Libya..
uu wa kanisa la Coptic Taarifa kutoka Misri zasema kuwa, ndege za kijeshi zimewashambulia wapiganaji wa jihadi nchini Libya kwa mabomu, baada ya kutolewa kwa mkanda wa video ulioonyesha wakristo wa Misri wa madhehebu ya Coptic wakikatwa shingo.
Jeshi la Misri linasema kuwa limelenga kambi za Islamic State, kituo cha mafunzo na maghala ya silaha, katika shambulizi hilo la mapema leo alfajiri.
Walioshuhudia wanasema kuwa, mji wa Derna ulioko mashariki mwa Libya na ambao umetekwa na wapiganaji wa jihadi ndio ulioshambuliwa vibaya.
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi, amesema kuwa mashambulio hayo ya angani ni jibu kwa wapiganaji hao ambao walitoa mikanda hiyo ya video hapo jana jumapili ilioOnyesha waumini kumi kati ya 21 waliotekwa nyara wakichinjwa.
Waumini hao wa madhehebu ya Coptic walikuwa wametekwa nyara majuma kadha yaliyopita.
Jeshi la Misri limetoa taarifa kwa vyombo vya habari inayosema kuwa raia wa taifa hilo walioko mbali ama karibu, wanafaa kuelewa kuwa wana jeshi la taifa linalowalinda kokote waliko. Taarifa kutoka Misri zasema kuwa, ndege za kijeshi zimewashambulia wapiganaji wa jihadi Nchini Libya kwa mabomu, baada ya kutolewa kwa mkanda wa video ulioonyesha wakristo wa Misri wa madhehebu ya Coptic wakikatwa shingo.
Jeshi la Misri linasema kuwa limelenga kambi za Islamic State, kituo cha mafunzo na maghala ya silaha, katika shambulizi hilo la mapema leo alfajiri.
Walioshuhudia wanasema kuwa, mji wa Derna ulioko mashariki mwa Libya na ambao umetekwa na wapiganaji wa jihadi ndio ulioshambuliwa vibaya.
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi, amesema kuwa mashambulio hayo ya angani ni jibu kwa wapiganaji hao ambao walitoa mikanda hiyo ya video hapo jana jumapili ilioOnyesha waumini kumi kati ya 21 waliotekwa nyara wakichinjwa.
Waumini hao wa madhehebu ya Coptic walikuwa wametekwa nyara majuma kadha yaliyopita.
Jeshi la Misri limetoa taarifa kwa vyombo vya habari inayosema kuwa raia wa taifa hilo walioko mbali ama karibu, wanafaa kuelewa kuwa wana jeshi la taifa linalowalinda kokote waliko.
Rais wa Misri alikuwa amesema nchi yake ina haki ya kujibu mashambulio kwa namna yoyote ile inayoona inafaa katika kulipiza kisasi cha mauaji ya kundi la Wakristo wa madhehebu ya Coptic yaliyofanywa na kikundi cha wapiganaji wa jihad nchini Libya wenye uhusiano na kikundi cha Islamic State.
Rais Abdel Fattah al-Sisi ametoa kauli yake kupitia televisheni ya taifa baada ya video moja kuonyesha mateka wapatao kumi wa kundi la waumini wa madhehebu ya Coptic kukatwa vichwa.
Waumini ishirini na mmoja wa madhehebu ya Coptic nchini Misri walitekwa nchini Libya wiki kadhaa zilizopita. Maandishi yaliyowekwa katika video hiyo yanaonyesha walilengwa kwa sababu ya dini yao. Misri imetangaza wiki moja ya maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo vya watu hao.
Mamlaka ya Kiislam inayoongoza nchini Misri,-- Al Azhar -- imeshutumu mauaji hayo na kuyaita ni ya "kinyama". Maelfu ya Wamisri wamekuwa wakivuka mpaka kwenda kutafuta kazi nchini Libya licha ya ushauri wa serikali yao ya Misri kuwakataza wasiende huko.
Watoto wanashiriki mzozo wa Sudan Kusini..
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu, Human Rights Watch limezituhumu serikali ya sudan kusini pamoja na vikosi vya waasi nchini humo kwa kuwasajili watoto walio na umri wa miaka 13 kupigana katika vita vya kiraia nchini humo.
Katika ripoti hiyo ambayo serikali imekana, Human Rights Watch limesema serikali imekuwa kiwasajili watoto hao, mara nyingi kwa nguvu, huku waasi waliwatumia watoto katika mzozo wa nchi hiyo ambao umeendelea kwa miezi 14 sasa.
Mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za kibinadam la human rights watch daniel bekele, amesema kuwa licha ya kuwepo na ahadi kati ya serikali na upinzani ya kuacha kutumia watoto kama wanajeshi, pande zote mbili bado zinaendelea kuwasajili watoto jeshini.
Waziri wa habari wa Sudan Kusini Michael Makuei amepuuzilia mbali ripoti hiyo na kusisitiza kwamba kuna watu wengine wazima wenye uwezo wa kusajiliwa au kuajiriwa jeshini.
Lakini shirika hilo la Human Rights Watch limesema kuwa vikosi vya serikali vinachukua watoto , katika tukio moja shirika hilo limedai kuwa baadhi watoto huchukuliwa nje ya makao ya umoja wa mataifa iliyoko kaskazini mwa nchi hiyo mjini Malakal.
Malakal, ni mji wenye utajiri wa mafuta, umebadilisha mamlaka mara sita tangu kuanza kwa vita Desemba mwaka wa 2013, vita ambavyo vimesababisha raia takriban 21000 kutafuta makaazi katika kambi za muda za umoja wa mataifa.
Mji huo wa malakal kwa sasa uko chini ya udhibiti wa serikali.
Shirika la umoja wa mataifa la unicef limesema mwaka uliopita watoto 12,000, wengi wao wavulana, walisajiliwa kujiunga na jeshi, la serikali au kulazimishwa kuwa wapiganaji wa waasi na wanamgambo washirika wa serikali.
Kuanzia mwanzoni mwa mwaka, huu shirika la Unicef, limefaulu kuandaa mazungumzo na kundi la waasi linaloongozwa na David Yau Yau na kuezesha kuachiliwa huru kwa watoto 3000, lakini watoto wengi wangali wanatumiwa na pande hizo mbili.
Kufuatia shinikizo la kimataifa, serikali ya sudan kusini imepitisha sheria mpya inayopiga marufuku watoto kuajiriwa au kusajiliwa jeshini kabla ya umri wa miaka kumi na nane.
Vita vilianza desemba 2013 nchini humo baada ya rais wa nchi hiyo salva kirr kumtimua makamu wake riek machar kwa madai ya kujaribu kupindua serikali..
Ebola:Shule zafunguliwa Liberia..
Kuanzia leo shule nchini Liberia zinaendelea kutoa mafunzo baada ya kufungwa kwa miezi kadhaa kufuatia mlipuko wa Ebola.
Huku kukiwepo vifo vya karibu watu 4000, Liberia imekuwa nchi iliyoathirika zaidi katika nchi tatu zilizogubikwa na janga hilo,
lakini wiki kadhaa zilizopita maafisa wa serikali wameamua kwamba kupungua kwa visa vipya vya maambukizi kunatoa nafasi ya kufunguliwa upya shule hizo.
Lakini wakati watoto wengi wanaelekea madarasani, hatua za kiafya zilizochukuiwa kudhibiti ugonjwa huo zimesababisha baadhi ya wanafunzi kutojumuika na wenzao kwa mafunzo.
Shule zimefunguliwa tena nchini Liberia, baada ya kufungwa kwa miezi kadhaa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa ebola.
Muhula mpya umeanza rasmi siku moja tu baada ya marais wa Liberia na Sierra Leone, kufanya ziara ya kwanza katika nchi za ngambo.
Wawili hao walihudhuria mkutano wa kimataifa nchini Guinea ambako waliapa kutokomeza ugonjwa huo kufikia aprili mwaka huu.
Afisa mmoja wa shirika la umoja wa mataifa la masuala ya watoto UNICEF amesema kuwa wanafunzi wengi wamerejea shuleni mapema hii leo na alishuhudia jinsi waalimu katika shule kadhaa wanavyochukua hatua za tahadhari.
Wanafunzi walilazimishwa kunawa mikono yao kabla ya kuingia darasani huku viwango vya joto vikichukuliwa kutoka kwa kila mwanafunzi.
Waalimu pia waliwaeleza wanafunzi jinsi ya kujikinga na ugonjwa huo wa ebola.
Shirika la UNICEF limekuwa mstari wa mbele kuhamasisha jamii kuhusiana na mbinu za kuzuia ugonjwa huo ambao umesababisha vifo vya zaidi ya watu elfu tisa katika mataifa ya Guinea, Sierra Leone na Liberia.
Rais wa Guinea Alpha Conde , Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia na Ernest Bai Koroma wa Sierra leone, wameungana pamoja na kutoa taarifa ya pamoja wakisema nia yao ni kutokomowza ugonjwa huo katika kipindi cha siku sitini.
Hata hivyo, kumekuwa na visa vipya vya maambukizi nchini Guinea katika siku za hivi karibuni.
Mwezi huu pekee watu sitini walipatikana na virusi vya ebola, na nchini Sierra Leone shirika la afya duniani limesema watu sabini na sita waliambukizwa.
Liberia ndio nchi iliyoshuhudia visa vingi vya ugonjwa huo na ndio nchi iliyoadhirika zaidi.
Shirika la UNICEF na mashirika mengine yametoa vifaa elfu saba mia mbili vitakavyotumika katika shule elfu nne nchini Liberia.
Zaidi ya waalimu elfu kumi na tano na wakuu wa shule mbali mbali nchini humo pia wamefunzwa mbinu
za kuzuia na kujikinga kutoka na virusi vya Ebola.
Katika nchi jiranai ya Guinea zaidi ya watoto milioni moja nukta tatu wamerejea shuleni hii leo.