Menu - Pages
▼
Monday, 23 February 2015
Bwana harusi aanguka kifafa kabla ya harusi..
Bi harusi mmoja kaskazini mwa nchi ya India alifanya maamuzi ya papo kwa hapo kuolewa na mmoja wa wageni waliofika kushereheka naye katika harusi yake baada ya mumewe kuugua ghafla.
Mwanamke huyo ajulikanaye kama Indra anayetokea Rampur jimbo la Uttar Pradesh, inaelezwa kuwa sekunde chache kabla ya ndoa ya wawili hao mume akaanguka kifafa, na hivyo kumlazimu kuondoka harusini na kwenda kumwona daktari.
Bi harusi Indra, alishikwa na hasira ya hali ya juu, kwakuwa mume alimficha juu ya hali yake, naye hakuwahi kujua hata siku moja kuwa , jamaa ana tatizo la kuanguka kifafa.
Indra akatoa ombi lake kuwa anahitaji kuolewa na mmoja wa wana familia ya bwana harusi , ambaye alikuja harusini kusherehekea harusi ya nduguye,na Indra akamtaka achukue nafasi ya nduguye badala yake, jamaa akaona nyota ya jaha imemuangukia, si akakubali !
Ndoa ikafungwa, hali ya bwana harusi wa kwanza mwenye kuanguka kifafa, haijajulikana mpaka harusi ya pili ilipokwisha.
Al Shabaab yatishia kushambulia Ulaya
Waziri wa Usalama wa Marekani anasema analitia maanani sana tishio la kundi la Waislamu wa Somalia, Al Shabaab, kwamba litashambulia maeneo ya maduka huko Marekani, Canada na Uingereza.
Katika mahojiano kwenye televisheni, Jeh Johnson alisema pametokea mabadiliko katika vitisho vya makundi ya wapiganaji Waislamu ambayo sasa yanatoa wito kwa washabiki wao katika nchi maalumu kufanya mashambulio.
Ulinzi umezidishwa kwenye eneo moja la maduka la Marekani katika jimbo la Minnesota, ambalo lina wakaazi wengi Wasomali
Mwaka wa 2013, shambulio lilofanywa na Al Shabaab dhidi ya eneo la maduka la Westgate mjini Nairobi, Kenya, liliuwa watu zaidi ya 60.
Al-Sisi,aomba msaada dhidi ya IS.
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amesema kuna haja majeshi ya muungano wa jumuiya ya kiarabu ya Pan-Arab kutoa majeshi yao ili kukabiliana na ugaidi.
Amesema kuwa mataifa kadhaa yametoa majeshi yao kukabiliana na kundi la wapiganaji wa Kiislam wa Islamic State tangu kuuawa kwa Wakristuhuko nchini Libya. Mataifa yaliyotoa misaada ya kifedha na kijeshi ni Jordan,Falme za Kiarabu na Marekani kwa lengo la kuangamiza kundi hilo Syria na Iraq. Akizungumza kupitia Televishen Sisi amesisitiza misaada ya kifedha kutoka mataifa ya Saud Arabia ambao walisaidia wakati wa kuuangusha utawala wa aliyekuwa Rais wa Kiislam wa Mohammed Morsi.
500 waokolewa machimboni Afrika Kusini
Inakadiriwa kuwa wachimbaji wapatao mia tano wameokolewa na magari ya zima moto kutoka machimboni baada ya kuwa wamebanwa chini ya mashimo yenye kina kirefu katika machimbo ya madini nchini Afrika Kusini.
Moto mkubwa uliripuka mapema mwanzoni mwa wiki hii umbali wa zaidi ya kilomita mbili katika machimbo ya mgodi wa Kusasalethu Magharibi mwa mji wa Johannesburg.
Mmiliki wa mgodi huo ni kampuni ya Harmony Gold wameeleza kuwa waliwaokowa wanaume zaidi ya mia nne na themanini na sita waliokuwa zamu siku hiyo .
Moto huo unasadikiwa ulianza wakati wa kazi ya matengenezo ilipokuwa ikiendelea.
Mwaka wa jana mgodi huo ulifungwa kwa muda wa wiki mbili ili kuwaondoa wachimbaji haramu ambao waliuvamia mgodi huo ambao wanshukiwa kuwa wao ndio walioanzisha moto huo.