Bi harusi mmoja kaskazini mwa nchi ya India alifanya maamuzi ya papo kwa hapo kuolewa na mmoja wa wageni waliofika kushereheka naye katika harusi yake baada ya mumewe kuugua ghafla.
Mwanamke huyo ajulikanaye kama Indra anayetokea Rampur jimbo la Uttar Pradesh, inaelezwa kuwa sekunde chache kabla ya ndoa ya wawili hao mume akaanguka kifafa, na hivyo kumlazimu kuondoka harusini na kwenda kumwona daktari.
Bi harusi Indra, alishikwa na hasira ya hali ya juu, kwakuwa mume alimficha juu ya hali yake, naye hakuwahi kujua hata siku moja kuwa , jamaa ana tatizo la kuanguka kifafa.
Indra akatoa ombi lake kuwa anahitaji kuolewa na mmoja wa wana familia ya bwana harusi , ambaye alikuja harusini kusherehekea harusi ya nduguye,na Indra akamtaka achukue nafasi ya nduguye badala yake, jamaa akaona nyota ya jaha imemuangukia, si akakubali !
Ndoa ikafungwa, hali ya bwana harusi wa kwanza mwenye kuanguka kifafa, haijajulikana mpaka harusi ya pili ilipokwisha.