Tuesday, 26 May 2015

Papa Francis: Sijatazama Tv kwa miaka 25.


Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, amesema kuwa hajawahi kutazama runinga kwa miaka 25 sasa.
Papa Prancis ambaye amewatamausha wachanganuzi wa kanisa hilo kwa kususia maisha ya kifahari katika makao makuu ya kanisa Vatican alisema alitizama runinga mara ya mwisho tarehe 15 mwezi julai mwaka wa 1990.
Alikoma kutizama runinga baada ya kumuahidi maria mtakatifu kuwa angekoma kushiriki uraibu huo.

Isitoshe raia huyo wa Argentina amesema kuwa hatumii mtandao wa intaneti.
Na akitaka kupata habari za kimataifa , Papa anasema kuwa huwa anatenga dakika 10 tu ya muda wake kusoma gazeti la kiitaliano.

Papa Francis vilevile anafuatilia habari za klabu yake maarufu huko Argentina kupitia kwa wahudumu wake ambao humsimulia yanayojiri.
Je unaweza kukaa mbali na Runinga yako Simu yako ama mtandao wa Intanet japo kwa siku moja ?
Share:

Jela siku 1 iwe ilani ya Ufisadi China.


Maafisa wa serikali Mashariki mwa China wamelazimika kuzuru gereza moja nchini humo kama ilani ya kutoshiriki ufisadi.
Maafisa hao 70 wakiwa wameambatana na wachumba wao walilazimishwa kushinda mchana kutwa katika gereza moja lililoko mjini Shiyan katika mkoa wa Hubei tarehe 15 mwezi Mei.
Serikali kuu ya China ilianzisha harakati za kukabiliana na ufisadi miongoni mwa wafanyikazi wa uma tangu rais aliyeko madarakani Xi Jinping alipochukua mamlaka mwaka wa 2012.

Tangu mwaka huo 2012, maelfu ya wafanyikazi wa uma wamechunguzwa na asilimia kubwa yao kuhukumiwa jela baada ya kupatikana na hatia ya kutumia madaraka yao vibaya.
Ziara hiyo ya lazima iligundulika baada ya shirika la kupambana na ufisadi kuchapisha ripoti hiyo katika jarida lake la hivi punde siku ya jumamosi.
Kulingana na ripoti hiyo ya tume ''ziara hiyo ilipaswa kuwaonya na kuwapa fursa ya kuonja maisha ndani ya jela nyuma ya vyuma vikubwa na madirisha yaliyoweka juu zaidi''
Picha zilizochapishwa zinaonesha maafisa hao wakuu wa umma wakiambatana na wachumba wao.

Maafisa hao walipata fursa ya kuzungumza na maafisa wanaotumikia vifungu tofauti kwa makosa ya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka yao.
Aidha walitembelea maonyesho ya picha na maandishi ya wafanyikazi wenza waliofungwa.
Tume hiyo ya kupambana na ufisadi CCDI ilisema katika ripoti hiyo kuwa wengi wa maafisa hao walipigwa na butwaa walipowaona maafisa waliowahi kufanya kazi pamoja na wengine wakawachwa vinywa wazi baada ya kuwatambua vigogo waliotamba katika enzi zao lakini sasa wakiwa ni wafungwa.

Maafisa hao walilazimishwa kusikiza sauti za maafisa waliowatangulia wakikiri makosa yao.
China imekuwa ikiendesha kampeini kubwa ya kupambana na ufisadi na ubadhirifu wa mal ya uma huku maafisa wa uma wakitakiwa kuishi maisha yao kadri ya mishahara yao.
Aisha wafanyikazi wa umma wametakiwa kukoma kupokea zawadi ghali kutoka kwa wanakandarasi na watu wenye nia ya kufanya biadhara na serikali.
Vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti visa ambayo maelfu ya wafanyikazi wadogo serikalini wanakamatwa na kilele cha kampeini hiyo dhidi ya ufisadi ilikuwa kukamatwa kwa aliyekuwa mkuu wa usalama wa ndani Zhou Yongkang.

Share:

Wimbi la Joto lawaua watu 430 India.


Takriban watu 430 wamekufa kutokana na wimbi la joto linalovuma nchini India.
Watafiti wamesajili kiwango cha juu mno cha nyuzijoto 48'C katika maeneo mengi nchini humo.
Vifo vingi zaidi vimeripotiwa katika majimbo ya kusini ya Telangana na Andhra Pradesh, ambapo watu 140 wamepoteza maisha yao kuanzia jumamosi wimbi hilo la joto lilipotokea.
Mji wa Allahabad ulioko Uttar Pradesh ulisajili vipimo vya nyuzijoto 48C huku wakaazi wa mji mkuu wa India New Delhi ukistahimili kiwango cha nyuzijoto 44C .

Maafisa wa utawala nchini humo wameanza kampeini ya kuwahamasisha wanainchi kukaa majumbani mwao na kuwashauri wanye waji mengi.
Yamkini viwango vya joto vimekuwa juu zaidi katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita lakini vifo vimeanza kuripotiwa mwishoni mwa juma.
Jimbo la Andhra Pradesh ndilo lililopoteza watu wengi zaidi ikiwa na jumla ya watu 246 waliopoteza maisha yao kuanzia juma lililopita.

"asilimia kubwa ya wale waliopoteza maisha ni watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50 walioshinda nje ya majumba yao.'' alisema kamishna wa kupambana na majanga katika jimbo la Andhra Pradesh.
Wakfu wa waandishi wa habari wanasema kuwa watu 186 wameaga katika wilaya 10 za jimbo la Telangana.
Watu 58 wamekufa kuanzia siku ya jumamosi.
Idara ya utabiri wa hali ya hewa imesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa hali hiyo ya joto kuendelea kwa siku kadha zijazo.

Watu wengine kumi walpoteza maisha yao katika jimbo la Magharibi mwa Bengal.
Waendesha teksi ambazo hazina kiyoyozi hawataruhusiwa kuhudumu kwa saa tano katika mji mkuu wa Kolkata. Hii inafuatia vifo vya madereva wawili.
Idara ya utabiri wa hali ya hewa inasema kuwa hali hiyo ya juu ya joto inatokana na ukosefu wa mvua.
Share:

Mafuriko yaua 18,Texas Marekani.


Mafuriko yamesababisha vifo vya watu 18 Magharibi mwa Marekani na Kaskazini mwa Mexco.
Wengi wa waliothibitishwa kufariki dunia kutokana na mafuriko hayo ni kutoka mpakani mwa Mexco katika mji wa Acuna.
Hata hivyo katika mji wa Texas watu watatu wamearifiwa kufa pia na wengine 12 hawajulikani waliko baada ya makazi yao kusombwa na mafuriko.
Gavana wa Texas Greg Abbott anasema mafuriko hayo yameleta madhara makubwa katika jimbo lake.
Share:

Urusi yaanzisha mazoezi ya Kijeshi.


Urusi imeanza mazoezi makali ya kivita yanayojumuisha kikosi cha anga cha wanajeshi 150 pamoja nakikosi cha mashambulio ya mbali ya makombora.
Wizara ya mambo ya ndani ya Urusi inasema kuwa wanajeshi 12,000 wanatarajiwa kuhusishwa na mazoezi hayo makali ya siku nne yanayolenga kutaka kujua uimara wa jeshi hilo na utayari wake.
Mazoezi hayo makali yanakuja sawa nay ale yanayoendeshwa na vikosi vya NATO na majeshi ya Ulaya Nordic yanayojumuisha zaidi ya wapiganaji 100 wa jeshi la anga.
Hata hivyo tukio hili la mazoezi ya majeshi ya Urusi yanaleta kwa nchi za magharibi kufuatia machafuko yanayoendelea Ukraine ambapo Urusi imekuwa ikinyooshewa kidole kutokana na machafuko hayo.
Share:

Ufisadi:Mawaziri 4 kushtakiwa Kenya


Kutumia ujumbe kwa vyombo vya habari, mkuu wa mashtaka ya umma nchini Kenya Keriako Tobiko, hii leo amevumbua yaliyomo katika hati za kesi za mawaziri wanne.
Tume ya maadili na kupambana na ufisadi ya Kenya imependekeza waziri wa uchukuzi mMhandisi Michael Kamau na waziri wa leba Kazungu Kambi kushtakiwa na matumizi mabaya ya ofisi.
Mhandisi Michael Kamau anakumbwa na shutuma za kutumia fedha ubadhirifu wa fedha za umma na kufanya mabadiliko katika ubunifu wa barabara ambayo tiyari ilikuwa imetengenezwa na mashauri.
Kazungu Kambi naye anadaiwa keteuwa wanachama wawili katika bodi ya shirika la taifa la hazina ya uzeeni kinyume na sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari jana alasiri jumapili, afisa mkuu wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi Halakhe Waqo, alisema kwamba mawaziri wanne waliochunguzwa ni waziri wa Uchukuzi Mhandisi Michael Kamau, waziri wa ardhi, makao na ustawi wa miji bi Charity Ngilu, waziri wa kilimo Felix Kosgei, waziri wa leba Kazungu kambi, seneta wa Nairobi Mike Sonko na mbunge .
Tume hio imemwandikia rais Uhuru Kenyatta ombi la kuongeza muda wa uchunguzi wa kesi zilizobaki.
Siku sitini ambazo walikuwa wamepewa kukamilisha uchunguzi wa ripoti hiyo zimetimia leo.

''Tumekuwa na shinikizo la kukamilisha kesi kwa wakati uliotolewa ila wajibu wetu wa kufanya uchunguzi wa kina ambao unaweza kustahimili uchunguzi mahakamani umetulazimu kuomba muda zaidi''alisema Halakhe Waqo
Kwa sasa tume hio imekamilisha kesi 56 kati ya 124 zilizowasilishwa kwa uchunguzi zaidi baada ya ripoti yao ya awali iliyokabidhiwa rais Kenyatta kuwasilishwa bungeni .
Kesi 21 tayari zimefikishwa kwa mkuu wa mashtaka ya umma Keriako Tobiko.
Kufikia sasa maafisa 19 wamefikishwa mahakamani na wengine 29, kulingana na afisa mkuu wa EACC, watafikishwa mahakamani siku chache zijazo katika maeneo kadhaa nchini yakiwemo Turkana, Machakos, Nyamira, Nairobi na Trans nzoia
Hata hivyo tume hii nayo pia imekumbwa na malumbano ya ndani kwa ndani ya shtuma za ufisadi, zilizosababisha kuchunguzwa kwa kiongozi wa tume hiyo na baadhi ya wanatume wake ambao hatimae walijiuzulu.
Share:

Basi lachomwa Burundi.


Basi moja la uchukuzi limechomwa moto mjini Bujumbura Burundi na waandamanaji waliorejea mabarabarani kupinga uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Waandamanaji wanachoma moto magurudumu haswa katika eneo la Kanyosha.
Kitongoji hicho kimekuwa kitovu cha maandamano haya dhidi ya awamu ya tatu ya rais Nkurunziza.

Mwandishi wa BBC mjini Bujumbura Ismael Misigaro amesema milio ya risasi inasikika mjini humo.
Maandamano haya yanarejea baada ya kuuawa kwa kiongozi wa chama cha upinzani Zedi Feruzi nje ya nyumba yake katika mji mkuu Bujumbura.
Aidha wanaharakati wa upinzani nchini humo wamesitisha mazungumzo na serikali rais Pierre Nkurunziza ya kutaka kutanzua mzozo ulioko wa kisiasa.

Mzozo huo unafuatia hatua ya Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu.
Uamuzi ambao wengi wanasema kuwa unaenda kinyume na sheria na ndio iliyosababisha kuwepo kwa jaribio la kumpindua, na maandamano ya wiki kadhaa.
Tayari zaidi ya raia 100,000 wa taifa hilo wametorokea mataifa jirani.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.