Monday, 17 November 2014

KIVUKO KIPYA CHA DAR-BAGAMOYO CHAPOKELEWA NA WAZIRI MAGUFULI....... Global Publisher

KIVUKO kipya kinachotegemea kufanya safari kati ya Jiji la Dar es Salaam na Bagamoyo kimepokelea leo na Waziri wa Ujenzi,John Magufuli katika Bandari ya Dar es Salaam.
Kivuko hicho mabacho kitakuwa kikipita katika vituo saba kati ya miji hiyo mwili, kimefungwa vyombo vya kuongozea vya kisasa (Navigational Equipment) vikiwemo GPS Compass, Automatic Identification System (AIS), Radar, Echo Sounder, CCTV Cameras na kina vyombo vya kutosha vya kuokolea watu kama ‘life jackets’, ‘life bouys’ na ‘life rafts’.
Akizungumza na GPL, Waziri Magufuli alisema” “Kuanza kwa kivuko hiki kutasaidia kwa kiasi kupunguza foleni kwa wakazi wa jijini la Dar es Salaam, kwani kina uwezo wa kubeba abiria 300 kwa kukaa.


Kivuko kipya cha MV Dar es Salaam-Bagamoyo.


 
 Waziri Magufuli akihutubia wadau waliofika katika sherehe hizo fupi katika Bandari ya Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa  wa Dar e s Salaam, Mecky Sadick, akizungumza na wadau bandarini.



Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema  akizungumza jambo.




 Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko (TEMESA) Japhet Massele, akitoa ufafanuzi kuhusu kivuko hicho.




 Sehemu ya ndani ya kivuko inavyoonekana.


Share:

Wito kwa wakazi kujihami dhidi ya Boko Haram..........BBC



Emir Sanusi alikuwa gavana wa benki kuu ya Nigeria kabla ya kuteuliwa kama Emir Kaskazini mwa Nigeria

Emir wa Kaskazini mwa Nigeria, ambaye ni mmoja wa viongozi wa kiisilmau wenye ushawishi mkubwa, ametoa wito kwa watu nchini humo kuchukua silaha na kujilinda dhidi ya mashambulizi ya kundi la wanamgambo wa kiisilamu wa Boko Haram.
Emir huyo wa Kano, Muhammad Sanusi, amewaambia wakazi wasisubiri wanajeshi kuwalinda kutokana na magaidi.
Emir huyo ambaye alikuwa gavana wa benki kuu nchini humo kabla ya kuchukua wadhifa wake wa Emir, alitoa matamshi yake ya kutatanisha kwenye mkutano wa maombi.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria amesema kauli kama hii sio kawaida kutolewa kwani Emir huyo huyo hazungumzii sana maswala ya kisiasa.




















Wapiganaji wa Boko Haram wamekuwa wakiwahangaisha wananchi kwa miaka mitano sasa
 
Wapiganaji wa wa Boko Haram wanaendelea kufanya mashambulizi ya mara kwa mara katika sehemu kadhaa za Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, huku wakiteka miji na mijiji ambko wamekuwa wakiwataka wakazi kufuata sheria kali ya kiisilamu.
Sanusi alikuwa mkosoaji mkuu wa serikali alipokuwa anafanya kazi yake ya benki, alisema kuwa watu hawapaswi kuogopa wanamgambo hao na kwamba wanapaswa kufanya wawezalo kujikinda kutokana na mashambulizi ya kundi hilo.
Mwandishi wa BBC anasema ingawa Emir huyo hakutaka kundi la Boko Haram, ilikuwa hatua ya kipekee kwa kiongozi kama huyo kuwataka watu kujihami dhidi ya Boko Haram.
Aanasema hii ni dalili tu ya mambo yalivyo nchini humo hasa katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.



Share:

Akana njama ya kumuua Mugabe..... source BBC



 
Makamu wa Rais Joyce Mujuru
 
Makamu wa Rais nchini Zimbabwe, anasema anapanga kuchukua hatua za kisheria dhidi ya shirika la habari la kitaifa kwa kumhusisha na njama ya kumuua Rais Robert Mugabe.
Joyce Mujuru amesema amewaamuru mawakili wake kumrejeshea hadhi yake ya kisiasa baada ya kuhusishwa na madai hayo ya uhaini pamoja na ufisadi.
Jarida la Sunday Mail la nchini humo, limeripoti kuwa kuna njama ya kumkodi mamluki kumuua Mugabe ili Bi Mujuru achukue mamlaka.
Mwezi jana Bwana Mugabe alifikisha miaka 90 na kusema hana nia ya kuachia madaraka.
Ametawala Zimbabwe tangu nchi hio kujipatia uhuru mwaka 1980.


 Rais Mugabe akiwa na mkewe Grace Mugabe

Rais Mugabe na Bi Mujuru walikuwa wandani wa karibui lakini kwa sasa wamehasimiana huku mjadala wa kumrithi Mugabe ukitokota katika chama tawala cha Zanu-PF kikijiandaa kwa kongamano lake la kitaifa mwezi ujao.
Mkewe Bwana Mugabe, Grace Mugabe amekuwa akiendesha kampeini dhidi ya Bi Mujuru akimtaka astaafu.
Amemtuhumu Bi Mujuru kwa kuwa mtu wa kishetani na mwenye kugawanya watu pamoja na kujipatia pesa kwa njia ya udanganiyifu, kutoka kwa makampuni.
Taarifa ya bi Mujuru akikana madai ya njama hiyo haikutarajiwa.
Ingawa hajaonyesha dalili za kuachia ngazi, anakabiliwa na shinikizo kali sana za kisiasa.
Jarida la Sunday mail liliripoti taarifa hizo za kushtua kwamba bi Mujuru na washirika wake wanapanga kumkodi mamluki ambaye atamuua Mugabe ili achukue mamlaka.
"ninakanusha madai hayo ya uhaini na ufisadi pamoja na kutumia vibaya mamlaka yangu, madai ambayo yamekuwa yakitolewa dhidi yangu kwa mda mrefu sasa,'' alisema Mujuru.
Amewataka mawakili wake kuchukua hatua za haraka za kisheria dhidi ya waliotoa madai hayo na kumharibia sifa yake.
Share:

Ebola yamuua daktari Marekani........BBC

 Daktari Salia alikuwa anafanya kazi nchini Sierra Leone na haijulikani ikiwa aliwatibu wagonjwa wa Ebola

 Daktari mmoja kutoka nchini Sierra Leone aliyekuwa anapokea matibabu ya Ebola nchini Marekani amefariki. Taarifa hii ni kwa mujibu wa hospitali ya Nebraska nchini humo. Daktari, Martin Salia mwenye umri wa miaka 44 na ambae ana uraia wa Marekani kutokana na ndoa yake kwa mwanamke mmarekani, aliwasili nchini humo kwa matibabu mnamo siku ya Jumamosi. Lakini Jumatatu asubuhi, hospitali ya Nebraska ilitangaza kuwa daktari huyo alifariki akipokea matibabu. Yeye ni mtu wa pili kufariki kutokana na Ebola nchini Marekani. Zaidi ya watu 5,000 wamefariki kutokana nba Ebola, tangu mlipuko wa ugonjwa huo kuripotiwa, wengi wao wakiwa katika mataifa ya Afrika Magharibi.

Eric Duncan raia wa Liberia alifariki kutokana na Eboka wakati akipokea matibabu nchini Marekani mwezi jana. Alikuwa amekwenda Marekani kuwatembelea jamaa wake. "tunasikitika sana kutangaza kuwa mgonjwa wa pili ambaye alikuwa anapokea matibabu ya Ebola, Dr Martin Salia, amefariki kutokana na ugonjwa huo kuwa katika hali iliyokuwa sugu kwa matiibabu,'' ilisema taarifa ya hopistali hiyo.

Wahudumu wa afya, walimsafirisha Dr Salia katika kituo cha afya cha Nebraska akiwa katika hali mbaya sana. Mkewe Salia alisema anashukuru kwa juhudi zilizofanywa kumtibu mumewe.
Alikuwa amefanya kazi kama daktari wa upasuaji katika hospitali ya Kissy United Methodist Hospital nchini Sierra Leone. Haijulikani ikiwa alihusika na kuwatibu wagonjwa wa Ebola.

Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.