Saturday, 29 November 2014

Rais Kikwete asema amepona Saratani.......


Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amesema amepona saratani baada ya kufanyiwa upasuaji mapema mwezi huu nchini Marekani.
Kiongozi huyo wa Tanzania mwenye umri wa miaka 64 ametoa hotuba kwa taifa kuelezea afya yake..
"Niligundulika kuwa na hatua ya pili ya saratani ya kibofu, ambayo baadaye ikaonekana kuwa ni hatua ya kwanza," alisema Kikwete katika hotuba iliyotangazwa moja kwa moja kupitia televisheni akiwa uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam baada ya kurejea kutoka Marekani.
Aliongeza kuwa madaktari wamesema sasa hali yake shwari: "Madaktari walisema saratani haikuenea katika sehemu nyingine za mwili na baada ya upasuaji sasa wamesema nimepona saratani."
Alisema aligundulika kuwa na saratani ya kibofu zaidi ya mwaka mmoja uliopita na alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Johns Hopkins Hospital tarehe nane Novemba.
Kikwete ambaye anamaliza muhula wake wa pili mwakani amesema wananchi wajenge tabia ya kupima afya zao ili wagundue maradhi mapema.
Share:

Nigeria:Raia watakiwa kuwa waangalifu.........


Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amewataka watu wote nchini Nigeria kuwa waangalifu na kushirikiana na vikosi vya usalama vya nchi hiyo ili kujaribu kuzuia mashambulizi zaidi yanayotekelezwa na wanamgambo wa Boko Haram kaskazini mwa nchi.
Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulizi hilo lililotokea kwenye msikiti mmoja mkubwa ulio kwenye mji wa Kano ambapo watu kadhaa waliuawa.
Hata hivyo shambulizi hilo linaaminika kutekelezwa na Boko Haram ambalo kampeni yake dhidi ya serikali imesababisha vifo vya maelfu ya watu mwaka huu.
Polisi walitibua njama ya shambulizi jingine kwenye mji ulio kaskazini mwa Nigeria wa Maiduguri ambapo mabomu sita yaliharibiwa ndani ya msikiti mmoja na kwenye soko lililo karibu.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.