Mario Balotelli ndiye mchezaji aliyebaguliwa sana katika ligi ya Uingereza ,huku mchezaji huyo akipokea zaidi ya ujumbe 8000 ,asilimia 50 zikiwa ni za kibaguzi.
Takwimu hizo za kushtua zimeripotiwa na Kick it Out ,ambao walibaini kwamba raia huyo wa Itali alilengwa sana katika mitandao ya Twitter huku mshambuliaji wa Arsenal Danny Welbeck akipokea ujumbe 1700 asilimia hamsini zikiwa za kibaguzi.
Mshambuliaji mwenza wa Balotelli katika kilabu ya Liverpool Daniel Sturridge pia alionekana kulengwa katika mitandao ya kijamii baada ya kupokea ujumbe wa 1600 asilimia 60 ikiwa ni ujumbe wenye mwelekeo wa kijinsia.
Utafiti huo pia umebaini kwamba kilabu ya Chelsea ndio kilabu iliobaguliwa zaidi kwa ujumbe 20,000 huku liverpool ikiwa ya pili na ujumbe 19,000 Arsenal ikiwa ya tatu kwa ujumbe 12,000 huku Manchester City na Manchester United zikipokea ujumbe 11,000.