Sunday, 23 November 2014

Kenya yauwa al-Shabaab 100.........source BBC


Makamo wa rais wa Kenya, William Ruto, anasema kuwa askari wa usalama wa Kenya wamewaandama wapiganaji wa al-Shabaab hadi kwenye kambi yao nchini Somalia, baada ya shambulio dhidi ya basi kaskazini-mashariki mwa Kenya hapo jana ambapo raia 28 waliuliwa.
Bwana Ruto alisema wapiganaji zaidi ya 100 waliuliwa katika operesheni mbili tofauti. Alisema kambi ya al-Shabaab iliangamizwa. Habari hizo hazikuthibitishwa na upande wa pili.
Gavana wa Mandera - ambako shambulio la jana lilitokea - amelaumu vikosi vya usalama kwa kushindwa kuwalinda raia. Alisema polisi kawaida wanashindwa kufanya uchunguzi kamili baada ya mashambulio.
Share:

Mauaji yanalenga kuzua uhasama wa kidini...........BBC

Baadhi ya miili ya abiria waliouawa na Al-Shabaab eneo la Mandera, Kenya.

Basi lililotekwa na Al-Shabaab eneo la Mandera likiwa njiani kuelekea Nairobi.


Mshauri wa ngazi ya juu wa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa mauaji ya watu 28 waliokuwa wakisafiri kwenye basi moja yalilenga kusababisha vita vya kidini nchini kenya.
Kwenye mahojiano na BBC Abdikadir Mohammed alitoa wito kwa wakenya kutoka imani zote kuungana pamoja dhidi ya kile alichokitaja kuwa vitendo vya uhalifu.
Wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab waliwapiga risasi wasafiri ambao hawangeweza kukariri Koran.
Al Shabaab ilisema kuwa shambulizi hilo lilikuwa la kulipiza kisasi mauji ya hivi majuzi ya waislamu yaliofanywa na wanajeshi wa Kenya kwenye mji wa pwani wa Mombasa.

Serikali ya Kenya imesema kuwa imeanza kuwatambua waliotekeleza mauaji hayo na itawafikisha mbele ya sheria hivi karibuni.
Share:

Wanamgambo wawateka watoto 10 Mali.........BBC


Maafisa wa kijeshi nchini Mali wanasema kuwa watu waliokuwa na silaha wamewateka nyara watoto kumi na kuwaua wawili ambao walijaribu kupinga kutekwa karibu na mji wa Kidal.
Afisa mmoja alisema kuwa watoto hao walilazimishwa kuwa wanajeshi.

Maeneo yanayozunguka mji wa Kidal yanadhibitiwa na kundi la kiislamu lililojitenga ambalo lilidhibiti eneo la kaskazini nchini Mali mwaka 2012 lakini baadaye likatimuliwa na wanajeshi wa Ufaransa kwa ushirikiano na vikosi vya muungano wa Afrika.
Share:

Boko Haram wauwa 100 hivi karibuni.........BBC


Ripoti kutoka kaskazini-mashariki mwa Nigeria zinaarifu kuwa kundi la wapiganaji Waislamu la Boko Haram, limefanya mashambulio mawili makubwa katika siku chache za karibuni ambapo watu karibu 100 wameuwawa.
Kiongozi mmoja katika jimbo la Borno alisema kuwa wapiganaji waliuwa wauza samaki karibu 50 karibu na kijiji cha Doron Baga, kando ya Ziwa Chad.
Alisema wapiganaji wa Boko Haram wameweka kizuizi kwenye njia ya kuelekea Chad na kuwakamata wachuuzi waliokuwa wakienda kununua samaki.
Katika tukio jengine hapo awali watu karibu 50 waliripotiwa kuwa waliuwawa karibu na mpaka wa Cameroon pale Boko Haram walipovamia kijiji cha Azara Kuya, siku ambapo soko huwa na watu wengi
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.