Makamo
wa rais wa Kenya, William Ruto, anasema kuwa askari wa usalama wa
Kenya wamewaandama wapiganaji wa al-Shabaab hadi kwenye kambi yao
nchini Somalia, baada ya shambulio dhidi ya basi kaskazini-mashariki
mwa Kenya hapo jana ambapo raia 28 waliuliwa.
Bwana
Ruto alisema wapiganaji zaidi ya 100 waliuliwa katika operesheni
mbili tofauti. Alisema
kambi ya al-Shabaab iliangamizwa. Habari
hizo hazikuthibitishwa na upande wa pili.
Gavana
wa Mandera - ambako shambulio la jana lilitokea - amelaumu vikosi vya
usalama kwa kushindwa kuwalinda raia. Alisema
polisi kawaida wanashindwa kufanya uchunguzi kamili baada ya
mashambulio.