Baadhi
ya miili ya abiria waliouawa na Al-Shabaab eneo la Mandera,
Kenya.
Mshauri
wa ngazi ya juu wa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa mauaji
ya watu 28 waliokuwa wakisafiri kwenye basi moja yalilenga
kusababisha vita vya kidini nchini kenya.
Kwenye
mahojiano na BBC Abdikadir Mohammed alitoa wito kwa wakenya kutoka
imani zote kuungana pamoja dhidi ya kile alichokitaja kuwa vitendo
vya uhalifu.
Wapiganaji
wa kundi la Al-Shabaab waliwapiga risasi wasafiri ambao hawangeweza
kukariri Koran.
Al
Shabaab ilisema kuwa shambulizi hilo lilikuwa la kulipiza kisasi
mauji ya hivi majuzi ya waislamu yaliofanywa na wanajeshi wa Kenya
kwenye mji wa pwani wa Mombasa.
Serikali
ya Kenya imesema kuwa imeanza kuwatambua waliotekeleza mauaji hayo na
itawafikisha mbele ya sheria hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment