Maafisa
wa kijeshi nchini Mali wanasema kuwa watu waliokuwa na silaha
wamewateka nyara watoto kumi na kuwaua wawili ambao walijaribu
kupinga kutekwa karibu na mji wa Kidal.
Afisa
mmoja alisema kuwa watoto hao walilazimishwa kuwa wanajeshi.
Maeneo
yanayozunguka mji wa Kidal yanadhibitiwa na kundi la kiislamu
lililojitenga ambalo lilidhibiti eneo la kaskazini nchini Mali mwaka
2012 lakini baadaye likatimuliwa na wanajeshi wa Ufaransa kwa
ushirikiano na vikosi vya muungano wa Afrika.
No comments:
Post a Comment