Mlipuko mkubwa umetokea katika mji wa Mogadishu nchini Somalia karibu na uwanja wa ndege.
Takriban
watu wanne wameuawa katika mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa ndani
ya gari karibu na msafara wa magari ya Umoja wa Mataifa mjini Mogadishu.Polisi wanasema kuwa bomu hilo lililipuka wakati msafara huo ulipokuwa unaelekea karibu na barabara iliyoko karibu na uwanja wa ndege mjin humo.
Mlipuko wa pili iliripotiwa kulenga vikosi vya muungano wa Afrika umbali wa kililomita 25 kutoka mjini humo ingawa taarifa bado ni finyu.
Duru zimearifu kuwa mlipuko huo huenda umesababishwa na mtu aliyejitolea muhanga aliyejilipua ndani ya gari.
Kundi la wapiganaji wa kiislamu la Al- Shaabab mara kwa mara hutumia milipuko ya magari, lakini kufikia sasa halijakiri kuhusika na mlipuko huo.
Kundi la Al-Shabab, ambalo limehusishwa na wapiganaji wa al-Qaeda, limekuwa likifanya mashambulizi ya mara kwa mara nchini Somalia na katika nchi jirani ya Kenya.
Mnamo siku ya Jumanne liliwaua watu 36 mjini Mandera karibu na mpaka na Somalia.
Hata hivyo bado halijatoa yamko lolote kuhusu shambulizi lililofanywa mjini Mogadishu.