Wednesday, 5 November 2014

Baada ya kushindwa vibaya kwa chama cha Democrat kwenye uchaguzi wa viti vya bunge la seneti nchini marekani rais wa marekani Barack Obama amewakaribisha viongozi wa baraza la congress kutoka vyama vyote katika ikulu ya White House siku ya ijumaa kujadili mwelekeo wa siasa za nchi hiyo.

Kutoweza kufanya kazi kwa pamoja baina ya rais na Congress kumezorotesha kupitishwa kwa miswada na viongozi wa Republican.
Seneta wa Republican na kiongozi wa walio wengi Mitch Mc Connell amepata tena kiti chake katika jimbo la Kentucky.
Chama cha Republican kimezoa viti vingi katika uchaguzi huo na kukifanya kuchukua udhibiti wa taasisi hizo muhimu dhidi ya kile cha Democrat.
Kiongozi wa zamani wa seneti kutoka chama cha Democratic , Harry Reid, amemuita Mitch McConnell kumpongeza na akasema ilikuwa ni wazi kwamba wapiga kura walitaka vyama vyote kushirikiana.

Mwenyekiti wa Kamati ya kitaifa ya Republican Reince Priebus amesema kuwa umma wa wamarekani umekiamini chama chake.
Share:

Watu wasiojulikani kwenye mji wa pwani nchini Kenya ,Mombasa wamemuua kwa kumpiga risasi kiongozi mashuhuri na mwenye msimamo wa wastani wa dini ya kislamu.

Sheikh Salim Bakari Mwarangi ambaye ni mwanaharakati wa kampeni dhidi ya itikadi kali alipigwa risasi wakati alipokuwa akirudi nyumbani kutoka msikitini jumanne usiku.
Viongozi sita wa dini ya kiislamu badhi yao wenye itikadi kali na wale walio na misimamo ya wastani wameuawa mjini Mombasa tangu mwaka 2012.
Eneo la pwani ya kenya lenye waislamu wengi limekumbwa na misururu ya mashambuli ya mabomu yanoyoaminika kutekelezwa na watu walio na uhusiano na kundi la Al shabaab lenye makao yake nchini Somalia.
Share:

Marekani imesema itapeleka rasimu ya maazimio ndani ya Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuweka vikwazo dhidi ya Watu wanaozorotesha hali ya kisiasa nchini Sudani Kusini... source-BBC

Rais wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ambaye ni Rais wa Australia amesema baadhi ya wanachama wa baraza hilo wanaunga mkono hatua ya kuwekewa vikwazo na kuzuia biashara ya silaha. Haijajulikana ni lini hatua hiyo itatekelezwa.
Mapigano yameendelea nchini Sudani Kusini ,ingawa kumekuwa na jitihada za kimataifa kuhakikisha makubaliano ya amani yanatekelezeka. Mzozo wa kuwania madaraka uliokuwepo kwa miezi kumi kati ya Rais Salva Kiir na aliyekuwa Makamu wake Riek Machar umegharimu maisha ya maelfu ya Watu na takriban watu milioni mbili kuyakimbia makazi yao.
Makubaliano ya amani yaliyotiwa saini yalishindwa, kwa kuwa pande zinazokinzana zilishindwa kuunda Serikali ya umoja
Share:

Hoteli moja ya kifahari ya wanyama wa kufugwa nyumbani imefunguliwa nchini Singapore.


Hoteli hiyo inatoa huduma kama vile vidimbwi vya kuoga vya wanyama hao,vyumba vyenye hewa safi na vyakula vya kuvutia, na hivyobasi kuimarisha viwango vya kuwabembeleza wanyama hao katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa.
Hoteli hiyo yenye urefu wa futi 4,317 kwa jina Wagington Hotel imejengwa katika nyumba za zamani za wakolini wa Uingereza zilizobadilishwa katika makaazi ya wanadiplomasia.
Vyumba vya kulalia katika hoteli hiyo vinagharimu dola 271 kwa mbwa watatu wanaotumia kwa pamoja chumba cha kifalme,kilicho na maeneo ya kifahari ya kuweka balbu,runinga,na vitanda vilivyotengezwa na ngozi.
Hoteli hiyo iliojengwa hususan kwa mbwa pia huwakaribisha paka.
''iwapo tunajitakia mema katika maisha yetu, kwa nini marafiki zetu walio waaminifu nao tusiwafanyie mambo mazuri'' aliuliza mmiliki wa hoteli hiyo Estelle Taylor.
''Kama watu tunaowapenda wanyama,tuna hisi kwamba ni vyema kuwa na eneo ambalo wanyama wanaweza kuwekwa ili nao wajisikie nyumbani'' aliongezea.
Wanaomiliki wanyama hao pia wanaweza kupata eneo la kufanya mafunzo,kunyoa, kukata kucha,kubadilisha rangi za wanyama hao pamoja na masaji.
Hoteli hiyo pia hutoa huduma ya gari la kifahari aina ya Limousine kwa wanyama hao kutoka makaazi yao hadi hoteli hiyo na kutoka hoteli hiyo hadi makaazi yao.
Nchini Singapore kuna zaidi ya maduka 250 ya wanyama, mengi yakiwa katika maduka makubwa ya jumla.


Mfanyibiashara mmoja hutoa huduma za kitalii kila wikendi ambapo wamiliki wa wanyama hao na wanyama wenyewe hutembezwa katika maboti.
Share:

Wapiganaji wa kundi la Boko Haram, wanashukiwa kuhusika katika shambulizi jingine huko mji Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Shambulio hilo lilitokea wakati wa mchana Nafada na kuharibu kituo cha polisi, benki na ofisi ya chama tawala cha (PDP).Mashahidi wa tukio hilo wanasema waliona miili ya wanajeshi watano. Kiongozi wa dini ya kiislamu wa eneo hilo ameuawa pia.
Mwandishi wa BBC anasema wanamgambo wa kundi hilo wamevamia maeneo mengi nakufanya Kaskazini Mashariki mwa Nigeria kuzidi kuanguka kutokana na mashambulizi hayo.
Mashambulizi hayo yanakuja siku baada ya kulipuliwa kwa bomu la kujitoa muhanga katika jimbo la Yobe na kuuwa zaidi ya watu kumi na tano.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.