Sunday, 7 December 2014

Wahamiaji 70 wafa maji Yemen.....















Watu 70 wamekufa baada ya boti iliyokuwa imejaza wahamiaji haramu kupinduka baharini, magharibi mwa Yemen.
Maafisa nchini Yemen wamesema wengi ya watu waliokuwa katika boti hiyo ni raia wa Ethiopia.
Hali mbaya ya hewa inaelezwa kwamba ndio chanzo cha kuzama kwa boti hiyo.
Mamia kwa maelfu ya wahamiaji wamekuwa wakihatarisha maisha yao kwa safari zisizo na usalama katika nchi zilizo katika pembe ya Afrika na Yemen kila mwaka.
Umoja wa Mataifa unamini kwamba kiasi cha watu watu mia mbili wamezama maji katika kipindi cha miezi kumi na mbili iliyopita.
Share:

Ndege iliyobeba silaha yakamatwa Nigeria...........

Ndege ya mizigo iliyosheheni silaha za kivita imekamatwa katika uwanja wa ndege wa Kano nchini Nigeria. Licha ya kukanusha awali, Urusi imesema inamiliki ndege ya mizigo iliyozuiwa katika uwanja wa ndege wa Kano kaskazini mwa Nigeria baada ya kugunduliwa imebeba silaha ambazo hazikuwa zimearifiwa. Hata hivyo, Msemaji wa Ubalozi wa Urusi nchini Nigeria, ambaye aliliambia Shirika la Habari la Urusi TASS kwamba wanamiliki ndege hiyo, amesema silaha hizo ni za kikosi cha kulinda amani cha Ufaransa.

Kwa mujibu wa Mwandishi wa habari wa BBC ndege hiyo bado inashikiliwa uwanjani hapo.
Awali, msemaji wa kikosi cha kulinda amani cha Ufaransa katika Jamhuri ya Afrika ya kati aliiambia BBC kwamba hawafahamu chochote kuhusu helikopta mbili, magari ya kijeshi na silaha nyingine zilizokuwa katika ndege hiyo.
Hata hivyo baadaye alipiga simu kufuta usemo wake kwa kusema kuwa ndege hiyo ilikuwa imebeba silaha kwa ajili ya wanajeshi wao, walioko katika kambi ya N’damena, ambazo zitapelekwa baadaye Ufaransa.

Msemaji wa Ubalozi wa Urusi mjini Abuja alisema pia ndege hiyo ni yao. Akitatanisha taarifa aliyoitoa awali kwamba ndege hiyo si yao. Kwa nini Ufaransa inatumia ndege ya Urusi kubeba silaha zake? na kwa nini ilisimama katika uwanja wa Kano, wakati ikiwa inaelekea nchi jirani ya Chad na hata Cameroun ikitokea Afrika ya kati? Kwanini baadhi ya silaha hazikuorodheshwa katika ndege hiyo kama zimebebwa?.
Hayo ni maswali yalioulizwa pande zote.

Seriakli ya Nigeria ambayo ndio muhusika mkuu wa tukio hilo, haijasema chochote.
Baadhi ya wachambuzi wanasema Nigeria inamiliki silaha hizo ilizonunua katika soko haramu. Wengine wanasema silaha hizo zilinunuliwa kutoka kwa waasi wa Seleka katika Jamhuri ya Afrika ya kati, wakielezea kwanini ndege hiyo imeingia nchini humo kutoka mji mkuu wa nchi hiyo, Bangui.
Nigeria imewekewa vikwazo vya silaha kutoka Marekani na nchi hiyo imekuwa ikiarifiwa kutumia njia zisizo halali kupata silaha kwa ajili ya kupambana na wapiganaji wa Boko haram.
Share:

MAANDALIZI YA SIKU YA UHURU YALIVYOPAMBA MOTO!........

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)MAANDALIZI ya siku ya uhuru wa Tanganyika (Tanzania Bara) Desemba 9, kutimiza miaka 53, yanaendelea Uwanja wa Uhuru ambapo kutakuwa na gwaride la kijeshi vikundi vya sanaa, kwaya, halaiki ya vijana, ‘brass band’ na matarumbeta.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, amesema milango katika Uwanja wa Uhuru itakuwa wazi kuanzia saa 12:00 asubuhi ambapo wananchi watakaofika katika hafla hiyo watatumia mlango wa kusini upande wa Barabara ya Mandela kuingia uwanjani, na waalikwa wenye kadi watatumoa mlango wa geti namba mbili 2 na viongozi watatumia geti namba tatu 3.


















Share:

Wafungwa wengi watoroshwa Nigeria..........















Watu waliokuwa na silaha wamevamia gereza katika mji wa Minna, katikati mwa Nigeria, na kuwaachilia huru wafungwa 200.
Walingia kwa nguvu kwenye jela Jumamosi katika jimbo la Niger.
Polisi wanasema haijulikani ikiwa uvamizi huo ulifanywa na kundi la wapiganaji Waislamu, Boko Haram, au gengi la wahalifu.
Boko Haram wamevamia magereza kadha katika miaka ya karibuni.
Share:

Ebola yauwa daktari mwengine S-Leone........


Wakuu wa Sierra Leone wanasema daktari mwengine amefariki kutokana na Ebola - ni daktari wa 10 kufa na ugonjwa huo.
Aiah Solomon Konoyima alifariki Jumamosi kwenye kituo cha matibabu karibu na mji mkuu, Freetown, siku moja tu baada ya wenzake wawili kufa na ugonjwa huo huo.
Mwezi wa Julai daktari maarufu kabisa kutibu wagonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone, Sheik Umar Khan, piya mwisho aliuliwa na virusi vya Ebola. Vifo 1,600 vya Ebola vimesajiliwa nchini humo.

Sierra Leone imekuwa ikijaribu kukarabati huduma za afya baada ya vita vikali vya wenyewe kwa wenyewe katika miaka ya 1990s. Na daktari kutoka Cuba ambaye alipona Ebola, ameahidi kuwa atarudi Sierra Leone kumaliza kupambana na ugonjwa huo nchini humo.

Dakta Felix Baez, ambaye alipata Ebola nchini Sierra Leone, alisema hayo aliporudi Havana baada ya kujaribiwa matibabu aina mpya nchini Uswiswi ambayo yalimponesha.
Dakta Baez alikuwa kati ya madkatari na wauguzi wa kwanza 250 walioambukizwa Ebola Afrika magharibi.

Cuba ndio nchi iliyotuma huko wafanyakazi wa utabibu wengi kabisa kwenda kupambana na Ebola.
Mchango huo wa Cuba umesifiwa kimataifa hata na Marekani, adui yake wa kisiasa.
Share:

Mutharika ajinyima nyongeza ya mshahara.......















Rais Peter Mutharika wa Malawi na naibu wake wameakhirisha kujipa nyongeza ya mishahara baada ya kuzuka malalamiko.
Nyongeza kutoka mshahara wa dola 3,000 na kufikia dola 5,000 kila mwezi, imezusha malalamiko nchini Malawi ambako pato la nusu ya wananchi halitimii dola moja kwa siku.
Bwana Mutharika na makamo wake, Saulos Chilima wamesema hawatojipa nyongeza ya mishahara hadi uchumi wa nchi utengenee.
Kabla ya viongozi hao kushika madaraka wafadhili walisimamisha msaada wa dola 150-milioni kwa sababu ya wasiwasi kuhusu rushwa.
Mishahara ya wabunge itazidishwa asili-mia-mia-tatu (300%)
Share:

Watu kadha wauwawa karibu na Beni DRC......















Inaarifiwa kuwa watu kama 30 waliuwawa katika mashambulio kwenye vijiji mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.
Inaarifiwa kuwa mashambulio hayo yalifanywa Jumamosi usiku kwenye vijiji karibu na mji wa Beni ambako watu zaidi ya 250 wameuwawa tangu mwezi Oktoba.
Wakuu na mashirika ya raia yanawalaumu wapiganaji kutoka Uganda wa kundi la ADF, lakini baadhi ya wadadisi wanasema hakuna ushahidi wa kutosha wa kuhusisha kundi hilo.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.