Sunday, 21 December 2014

Korea kazkazini sasa yaionya Marekani.


Korea Kazkazini sasa inataka uchunguzi wa pamoja na Marekani kufanywa kuhusu wizi wa mtandaoni uliosababisha kampuni ya Sony Pictures kuahirisha maonyesho ya filamu ya ucheshi inayomdhihaki raia wa Korea kazkazini Kim Jong-un.
Imesema kuwa shtuma hizo za shirika la ujasusi nchini marekani FBI kwamba Pyongyang ndio iliotekeleza uovu huo inaliharibia jina taiafa hilo.
Chombo rasmi cha habari nchini humo kilimnukuu waziri wa maswala ya kigeni ambaye jina lake halikutajwa akisema kuwa taifa lake litachukua hatua kali iwapo Marekani itakataa ombi hilo.
Taifa la Korea Kazkazini hapo awali lilikuwa limeunga mkono uvamizi huo wa kampuni ya Sony likisema kuwa ni kitendo cha haki.
Rais Obama amesema kuwa Marekani itajibu shambulizi hilo la mtandaoni wakati utakapowadia.
Share:

Wanaume 28 washtakiwa kwa uasherati..


Watu 28 wamefikishwa mahakamani mjini Cairo Misri kutokana na mashtaka ya uasherati katika kile kinachoonekana kama ishara za kampeni dhidi ya ushoga.
Baadhi ya washtakiwa walikuwa wakilia baada ya kufikishwa mahakamani wakiwa wamefungwa pingu.
Mmoja alilalama kwamba yeye na wafungwa wenzake walipigwa na polisi.
Wanaume hao walikamatwa mapema mwezi huu katika kidimbwi cha kuoga kwa jina hammam mjini Cairo.
Wanahabari wa chombo kimoja cha habari walichukua filamu ya uvamizi huo wa polisi.
Miezi miwili iliopita,watu wanane walifungwa miaka 3 jela baada ya kunaswa katika kanda ya video ambayo wakuu wa mashtaka wanasema ilionyesha wakifanya harusi ya watu wa jinsia moja mjini Cairo.
Share:

Kura zaanza kuhesabiwa Liberia.


Kura zimeanza kuhesabiwa nchini Liberia ambapo uchaguzi wa Useneta umefanyika licha ya mlipuko wa ebola.
Idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura ilikuwa chini huku watu wengi wakisalia majumbani mwao kwa hofu ya maambukizi ya ugonjwa huo.
Viwango vya joto vya wapiga kura vilichukuliwa ,huku wakiambiwa kusimama kwa umbali wa mita moja mmoja baada ya mwengine na kuosha mikono yao kabla ya kupiga kura na hata baada ya kushiriki katika shughuli hiyo.
Matokeo ya mapema yanatarajiwa baadaye siku ya jumapili.
katika mji mkuu wa Monrovia ,mwana wa rais Ellen Johnson Sirleaf anakabiliana na mwanasoka mkongwe George Weah ambaye aliwania urais mwaka 2005.
Share:

Somalia yawakataa wanajeshi wa S.Leone.


Wanajeshi wa kulinda amani kutoka Sierra Leone wameondoka nchini Somali na hakuna wanajeshi wengine wa taifa hilo watakaochukua mahala pao kufuatia wasiwasi wa ugonjwa wa Ebola.
Umoja wa Afrika una mpango wa kutafuta wanajeshi wengine kutoka mataifa yenye wanajeshi wake nchini humo.
Zaidi ya wanajeshi 800 wa Sierra Leone walio kusini mwa bandari ya Kismayu wameondoka kuelekea nyumbani.
Walitarajiwa kuondoka mapema lakini safari yao ikacheleweshwa kwa zaidi ya miezi sita baada ya mmoja wa wanajeshi wa Sierra Leone waliotarajiwa kuchukua mahala pao kupatikana na ebola
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.