Profesa Stephen Hawking, mmoja wa wanasayansi mahiri nchini Uingereza, amesema juhudi za kutengeneza mashine inayofikiria inatishia uwepo wa binadamu............>>>>>INGIA HAPA<<<<<
Tuesday, 2 December 2014
Mashine yenye uwezo wa kufikiri kitisho..........
Profesa Stephen Hawking, mmoja wa wanasayansi mahiri nchini Uingereza, amesema juhudi za kutengeneza mashine inayofikiria inatishia uwepo wa binadamu............>>>>>INGIA HAPA<<<<<
Wakuu wa usalama watimuliwa Kenya...........source BBC
Rais Uhuru Kenyatta amemwachisha
kazi waziri wa usalama Joseph Ole Lenku na kumpendekeza waziri mpya wa
usalama Joseph Nkaiseri kuchukua nafasi hio.
Wakati huohuo mkuu wa
polisi nchini Kenya inspekta generali David Kimaiyo amejiuzulu kutokana
na shinikizo dhidi yake afanye hivyo kwa kushindwa kukabiliana na utovu
wa usalama nchini.Rais Kenyatta alisema kuwa baada ya mazungumzo na Bwana Kimaiyo alikubali 'kustaafu' mapema kutoka kwa majukumu yake kwa sababu za kibinafsi.
Rais alitoa tangazo hilo wakati akihutubia taifa kufuatia shambulizi la hapo jana dhidi ya wachimba migodi 36 waliouawa na Al Shabaab mjini Mandera Kaskazini ya Kenya.
Rais pia alitangaza kuwa amekubali ombi la Generali wa polisi David Kimaiyo kuachia wadhifa wake.
Kimaiyo na Ole Lenku wamekuwa wakikabiliwa na shinikizo za kuachia ngazi kufuatia kukithiri kwa utovu wa usalama nchini.
Hatua ya kuwatimua kutoka katika nyadhifa zao wawili hao bila shaka litakuwa jambo la kuridhisha kwa wakenya wengi ambao wamekuwa wakilalamikia utovu wa usalama na kuwataka waondoshwe ofisini.
Uteuzi wa Joseph Nkaisery kama waziri mpya wa usalama ni jambo jipya kwani atakuwa mwanasiasa wa kwanza kutoka kwa upinzani kuwa ndani ya serikali.
Alipokuwa anahutubia nchi,Rais Kenyatta aliwasihi wabunge kuongeza mda wa vikao vyao vya leo ili kumhoji na kumkagua Nkaisery aliyeteuliwa kuchukua nafasi ya waziri mpya wa usalama na maswala ya ndani ili wamuidhinishe.
Al Shabaab waua 36 Mandera,Kenya................
Kundi
la wanamgambo nchini Somalia Al Shabaab limekiri kuwaua watu 36
katika shambulio lililotokea kwenye machimbo ya kokoto karibu na mji
wa Mandera kaskazini mwa Kenya.
Katika
taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa kundi hilo, wanamgambo hao
wamesisitiza kuwa ndio waliowaua wakenya hao kwa sababu ya majeshi ya
Kenya kuendelea kuwa nchini Somalia.
Taarifa
za mauaji hayo zilitolewa kwa mara ya kwanza na Shirika la Msalaba
Mwekundu.
Inaarifiwa
kuwa wafanyakazi hao walipigwa risasi wakiwa katika mahema ya.
Walioshuhudia shambulizi walisema kwamba wapiganaji hao waliwatenga
waisilamu na wakristo huku wakiwachinja baadhi, na kuwapiga risasi
wlaiosalia.
Wakazi
wa eneo hilo wamesema waathirika wote wa tukio hilo ni watu wasio
Waislam ambao walikuwa wakifanya kazi katika machimbo hayo yaliyopo
Kormey kilomita 15 kutoka mji wa Mandera Kaskazini mwa Kenya.
Tukio
hili linafuatia tukio la wiki moja iliyopita ambapo watu wapatao 28
waliuawa katika shambulio la basi la abiria huko Mandera.
Kundi
la wapiganaji wa Kiislam la Al Shabab wamekiri kuhusika na mauaji
hayo.
Mkuu
wa Polisi eneo hilo, amesema bado wanafuatilia tukio hilo.
Katika
tukio lingine, mtu mmoja ameripotiwa kuuawa nchini Kenya kufuatia
mlipuko katika klabu moja ya usiku katika mji wa Wajir kaskazini mwa
Kenya.
Kwa
mujibu wa Kamishna wa Polisi wa Wajir, Frederick Sishia, shambulio
hilo limefanyika saa mbili usiku na kuua mtu mmoja na watu wengine
wanne wamejeruhiwa.
Washambuliaji
hao walitumia magruneti na silaha nyingine za kijeshi kufanya
shambulio hilo.
Wiki
iliyopita watu wengi waliuawa eneo la Mandera kaskazini mwa Kenya.
Kenya
imejikuta ikilengwa na mashambulio ya kigaidi tangu majeshi yake
yapelekwe nchini Somalia kukabiliana na wapiganaji wa Al Shabab.
Mbali na miji ya kaskazini mwa Kenya kushambuliwa kila mara, miji
mikubwa nchini humo ya Nairobi na Mombasa imekuwa ikilengwa na
mashambulio ya kigaidi.
Kenyatta:Kenya haitatikiswa na magaidi.............
Rais
Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema kuwa Kenya haitachoka katika vita
vyake dhidi ya ugaidi kufuatia shambulizi lililofanywa dhidi ya
wachimba migodi mjini Mandera Kaskazini ya Kenya.
Ametoa
kauli hiyo katika hotuba yake kwa taifa baada ya shambulizi lengine
lililofanywa na kundi la wanamgambo la Al Shabaab dhidi ya wakenya
wasiokuwa na hatia.
Kundi
hilo liliwavamia wachimba migodi 36 waliokuwa katika machimbo ya
kokoto mjini Mandera.
Kundi
hilo liliwaua wakenya wengine 28 waliokuwa wanasafiri kutoka mjini
Mandera siku kumi zilizopita.
Kenyatta
amelaani wanamgambo hao wa Al Shabaab kwa kutaka kuigawanya Kenya
katika msingi ya kidini na kuwataka wakenya kuungana dhidi ya kile
alichokitaja vita dhidi ya ugaidi.
Kenyatta
aliwataka magaidi wa Al Shabaab kama wanyama walio na kichaa.
Aliwasihi
wakenya kuungana katika vita dhidi ya magaidi.
Siku
kumi zilizopita, Al Shabaab waliuwaua abiria 28 waliokuwa wanasafiri
kwa basi kutoka mjini Mandera karibu na mpaka na Somalia kuelekea
likizoni makwao. Wengi wa waliouawa walikuwa walimu wa shukle za
umma.
Jela miaka 50 kwa kuwaharibu watoto Kenya.........
Mahakama nchini Kenya imemhukumu kifungo cha miaka 50 jela raia mmarekani kwa kutengeza na kusambaza picha chafu za video za watoto wakifanya vitendo vya ngono.
Terry
Ray Krieger alikiri makosa yake mbele ya mahakama mwezi jana. Pia
alipatikana na kosa la kuwadhalilisha watoto wadogo huku akinasa
vitendo hivyo kwa kanda ya video.
Alikamatwa
na maafisa wa usalama Kenya baada ya kupata taarifa kutoka kwa
shirika la kimataifa la polisi kwamba alikuwa anasambaza video hizo
zilizokuwa zinaonyesha watoto wakifanyiwa vitendo vichafu kwenye
mtandao.
Krieger
amewahi kushtakiwa kwa makosa sawa na hayo na kufungwa jela nchini
Marekani miaka 20 iliyopita.
Polisi
wa Kenya walipokea taarifda kutoka kwa polisi nchini Marekanmi
wakiwaamiwa kuwa kuna raia mmarekani nchini Kenya anayetengeza na
kusambaza video chafu za watoto wadogo wakihishwa na vitendo vya
ngono.
Aliomba
mahakama kumuonea huruma kutokana na maradhi anayougua ya mifupa
lakini mahakama ilisema kuwa maradhi yake sio haiwezi kuwa sababu ya
kutowajibishwa kwa makosa yake.