Kundi
la wanamgambo nchini Somalia Al Shabaab limekiri kuwaua watu 36
katika shambulio lililotokea kwenye machimbo ya kokoto karibu na mji
wa Mandera kaskazini mwa Kenya.
Katika
taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa kundi hilo, wanamgambo hao
wamesisitiza kuwa ndio waliowaua wakenya hao kwa sababu ya majeshi ya
Kenya kuendelea kuwa nchini Somalia.
Taarifa
za mauaji hayo zilitolewa kwa mara ya kwanza na Shirika la Msalaba
Mwekundu.
Inaarifiwa
kuwa wafanyakazi hao walipigwa risasi wakiwa katika mahema ya.
Walioshuhudia shambulizi walisema kwamba wapiganaji hao waliwatenga
waisilamu na wakristo huku wakiwachinja baadhi, na kuwapiga risasi
wlaiosalia.
Wakazi
wa eneo hilo wamesema waathirika wote wa tukio hilo ni watu wasio
Waislam ambao walikuwa wakifanya kazi katika machimbo hayo yaliyopo
Kormey kilomita 15 kutoka mji wa Mandera Kaskazini mwa Kenya.
Tukio
hili linafuatia tukio la wiki moja iliyopita ambapo watu wapatao 28
waliuawa katika shambulio la basi la abiria huko Mandera.
Kundi
la wapiganaji wa Kiislam la Al Shabab wamekiri kuhusika na mauaji
hayo.
Mkuu
wa Polisi eneo hilo, amesema bado wanafuatilia tukio hilo.
Katika
tukio lingine, mtu mmoja ameripotiwa kuuawa nchini Kenya kufuatia
mlipuko katika klabu moja ya usiku katika mji wa Wajir kaskazini mwa
Kenya.
Kwa
mujibu wa Kamishna wa Polisi wa Wajir, Frederick Sishia, shambulio
hilo limefanyika saa mbili usiku na kuua mtu mmoja na watu wengine
wanne wamejeruhiwa.
Washambuliaji
hao walitumia magruneti na silaha nyingine za kijeshi kufanya
shambulio hilo.
Wiki
iliyopita watu wengi waliuawa eneo la Mandera kaskazini mwa Kenya.
Kenya
imejikuta ikilengwa na mashambulio ya kigaidi tangu majeshi yake
yapelekwe nchini Somalia kukabiliana na wapiganaji wa Al Shabab.
Mbali na miji ya kaskazini mwa Kenya kushambuliwa kila mara, miji
mikubwa nchini humo ya Nairobi na Mombasa imekuwa ikilengwa na
mashambulio ya kigaidi.
0 comments:
Post a Comment