Baraza makanisa nchini Kenya(NCCK) limewalaumu vongozi wa kiislamu na serikali kushindwa kuzuia mashambulizi dhidi ya wakristu.
Wakizungumzia mauaji yanayosemekana kutekelezwa na kundi la Al-Shabaab na kuwaua wakristu 28 Jumamosi asubuhi.Baraza hilo limesema kuwa halitafanya mazungumzo mengine na viongozi wa dini ya kiislamu kwa sababu wameshindwa kuwathibiti waumini wao ambao NCCK inadai kuwa wamekuwa wakiwashambulia wakristu kwa maeneo ya ibada na kwingineko.
Kwa siku nyingi baraza la makanisa limekuwa likichukua msimamo wa kadri kunapotokea mashambulizi nchini Kenya ama kwa jumla kuhusu suala la usalama.
Ila leo walikuwa na msimamo mkali sana kuhusiana na mauaji yaliyotokea Mandera wakalaumu kwana viongozi wa kiislamu kwa kutokuwa wakakmavu kuwashauri waumini wao.
Huyu hapa katibu Mkuu wa baraza hilo Peter Karanja alisema kuwa wamekuwa na mikutano mingi na viongozi wa dii ya kiislamu lakini kumekuwa na mshambulizi mengi yanyowalenga wakristu
Japokuwa walionyesha kukerwa na tukio la Mandera, viongozi hao wamesema kuwa serikali na viongozi wa kiislamu hawajashughulikia tatizo la vijana wanaoshikilia mismamo mikali ya dini katika maeneo ya Pwani na Kaskazini ya nchini ambao wamekuwa hatari kwa usalama
Hata hivyo viongozi wa kiislamu hawajachukulia kwa wepesi sula hilo. Dr Hassan Kinyua ambaye ni mkurugenzi wa masuala ya kidini katika baraza kuu la waislamu(SUPKEM) anataka NCCK iendelee kufanya mazungumzo na SUPKEM.
Ameongeza kuwa ni makosa kila mara kuhusisha suala la ugaidi na dini ya kiislamu
Lakini viongozi hao wanapoishambulia serikali hususan vikosi vya usalama kwa kulegea katika vita dhidi ya ugaidi Rais uhuru Kenyatta amewatetea maafisa wa usalama akisema kuwa suala la usalama ni la wakenya wote.
Na hata watu wanapotaka wakuu wa usalama wajiuzulu Rais Uhuru anasema vikosi vya usalama havitavumilia dini kutumia majengo ya ibada kuendeleza ugaidi
Hapo jana makundi kadhaa ya kutetea haki za binadamu yaliandamana yakimtaka Rais Uhuru Kenyatta kuwaachisha kazi wakuu wa uslama kwa kushindwa kuzuia mashmbulizi dhidi ya wakenya.
Kumekuwa na mashmbulizi mengi nchini Kenya tangu jeshi la Kenya liingie Somalia kuwakabili wanamgambo wa Al Shabaab ambao wanadhaniwa kuwa wamekuwa wakitekeleza mashambulizi nchini Kenya na kutorokea Somalia.
Baadhi ya mashambulizi makubwa kuwahi kufanyika lile la Westgate jijini Nairobi ambako zaidi ya watu sitini waliuawa na huko Mpeketoni katika pwani ya Kenya.
Serikali ya Kenya imesisitiza kuwa jeshi la Kenya liliwaua zaidi ya wapiganaji 100 wa Al-shabaab wanaodaiwa kuhusika na mauji ya watu 28 waliokuwa wakisafiri kwenye basi kutoka Mandera kuelekea katika sehemu nyingi za nchini ila baadhi wananchi wanatilia shaka kauli hiyo.