Maiti
za watu waliouliwa na al-Shabaab Jumamosi asubuhi nje ya mji wa
Mandera, Kenya, karibu na mpaka wa Somalia, zilipelekwa na wanajeshi
hadi mjini humo.
Serikali
ilikuwa inajitayarisha kusafirisha miili hiyo hadi mji mkuu, Nairobi.
Basi
lililokuwa limebeba abiria 60 lilitekwa nyara alfajiri na abiria 28
walipigwa risasi na kuuwawa.
Wengi
waliouwawa ni kutoka maeneo mengine ya Kenya ambao wakifanya kazi
Mandera.
Inasemekana
kuwa wengi wao walikuwa waalimu na wafanyakazi wa wizara ya afya
ambao walikuwa wanarudi nyumbani kuwa na familia zao wakati wa Noeli.
Msemaji
wa wapiganaji wa Somalia, al-Shabaab, alidai kuwa walihusika na
shambulio hilo.
Wanajeshi
na polisi wametumwa huko kwenda kuwasaka wale waliohusika na
shambulio hilo lakini hakuna taarifa kuwa wamekamatwa.