Shirika la kimataifa la misaada, Medecins Sans Frontieres, limeonya kwamba vifo vitokanavyo na kuumwa na nyoka huenda vikaongezeka. Hali hii inasababishwa na kuisha kwa akiba za dawa inayotibu sumu ya nyoka. Inadhaniwa kwamba watu laki moja huuawa na nyoka kila mwaka.
Wednesday, 9 September 2015
Vifo vinavyotokana na nyoka kuongezeka?
Shirika la kimataifa la misaada, Medecins Sans Frontieres, limeonya kwamba vifo vitokanavyo na kuumwa na nyoka huenda vikaongezeka. Hali hii inasababishwa na kuisha kwa akiba za dawa inayotibu sumu ya nyoka. Inadhaniwa kwamba watu laki moja huuawa na nyoka kila mwaka.
Mtoto aliyeibiwa apatikana baada ya miezi 4.
Mahakama nchini El Salvador imeamuru mtoto aliyebadilishwa punde baada ya kuzaliwa kukutanishwa na wazazi wake halisi miezi minne baadaye
Mahakama hiyo iliamuru uchunguziwa kina kufanyika kuhusiana na daktari aliyeshutumiwa na mama kwa kumbadilishia mtoto wake wakati wa kujifungua.
Mama huyo, Mercedes Casanella,anasema kwamba mtoto aliyemuona muda mfupi baada ya kujifungua mwezi May alikua na ngozi nyeupe na maumbile
tofauti na yule aliyekabidhiwa baadae .
Mtoto Mweusi
''Mtoto niliyemuona alikuwa na rangi ya hudhurungi lakini yule aliyeletwa alikuwa ni mweusi titi ti''
Kipimo cha vinasaba DNA kimethibitisha kwamba mtoto huyo mchanga si wa mwanamke huyo kibayolojia.
Bi Casanella anasema kuwa daktari huyo Alejandro Guidos alikuwa amekusudia kufanya mabadiliko hayo.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema kwamba matokeo ya uchunguzi wa vinasaba umebaini mtoto huyo si wa bi Casanella na mumewe.
Aidha hayo yalitiliwa pondo na matokeo ya uchunguzi uliofanywa kwa watoto wote waliozaliwa katika zahanati hiyo ya afya katika siku hiyo moja.
Wazazi wa mtoto huyo wamemshutumu dakatari , Alejandro Guidos, kwa kumuuza mtoto wao mweupe kwa wafanyabiashara haramu ya watoto , lakini alikana kufanya kosa lolote
Guterres aomba wakimbizi waruhusiwe Ulaya
Kamishna wa tume ya Umoja wa Mataifa, anayehusika na masuala ya wakimbizi, Antonio Guterres, ameyaomba mataifa ya Ulaya kuwakubali wakimbizi laki mbili wanaokimbia mapigano nchini Syria, Iraq na Afghanistan.
Bwana Guterres amesema kuwa jibu lao huenda likaathiri mustakabali wa muungano wa Ulaya.
Kamishna Guterres amewasihi viongozi wa Ulaya kutafuta namna ya kuwaruhusu wakimbizi halali kuingia Ulaya kwa urahisi.
Kamishna huyo wa Umoja wa Mataifa, ameonya kuwa nchi za Ulaya haziwezi kuendelea kushughulikia suala hili la wakimbizi kila moja kwa njia yake.
Amesema kuwa bara hilo likikosa kushikana kwa pamoja kuhusu suala hili watakaonufaika ni walanguzi wa binadamu na mawakala wa wahamiaji.
Awali wajumbe kutoka tume ya Ulaya, walianza ziara katika kisiwa cha Kos, nchini Ugiriki, ambako maelfu ya wakimbizi wamekuwa wakiwasili kila siku.
Wengi wa wakimbizi hao, wamelalamika kuwa inawachukua muda mrefu, kabla ya kupata stakabadhi wanazohitaji kuondoka kisiwani humo.
Serikali ya Ugiriki imeahidi kuharakisha shughuli hiyo, lakini kamishna wa Ugiriki, anayehusika na masuala ya uhamiaji amesema kuwa ni lazima mataifa yote ya Ulaya, yashirikiane kutafuta suluhisho la kudumu.
Ziara hii ya tume ya Ulaya, ndio ya punde zaidi katika msururu wa juhudi za kutafutia ufumbuzi janga la uhamiaji barani Ulaya.
Punda na farasi ni marufuku Nigeria
Jeshi la Nigeria limepiga marufuku matumizi ya farasi na punda katika jimbo la Kaskazini Mashariki la Borno, kama sehemu ya juhudi za vita dhidi ya Boko Haram .
Kundi hilo limekua likitumia farasi kutekeleza mashambulizi dhidi ya wanavijiji
Huku jeshi la Nigeria likionekana kupata mafanikio katika vita vyake dhidi ya Boko Haram, kundi hilo linaripotiwa kukabiliwa na kibarua kigumu kupata mafuta ya kuweka kwenye magari yake kwa hivyo hutumia farasi kwa usafiri mbadala.
Lakini tayari kuna marufuku ya matumizi ya piki piki ambazo zilikuwa zikitumiwa na wanamgambo wa Kiislamu wa Boko Haram kuwasafirisha wapiganaji wake katika mashambulizi.
Pikipiki hizo zilirahisisha kutoroka kwa washambulizi , kwa hivyo kwa sasa kuna hofu kwamba marufuku ya sasa itadhoofisha zaidi uchumi wa maeneo ya vijijini na kuathiri maisha ya watu wa kawaida.
Punda hutumiwa kwa kusafirishia bidhaa na mara nyingi farasi huendeshwa katika tamasha za kidini na kitamaduni.
Papa Francis kurahisisha sheria ya talaka.
Papa Francis anatarajia kurahisisha taratibu zinazoruhusu wafuasi wa kanisa katoliki waliooana kutoa talaka na kuolewa tena huku wakibakia kuwa wafuasi wa katika kanisa hilo .
Maelezo ya taratibu hizo yanatarajiwa kutangazwa mjini Vatcan baadaye leo .
Papa aliunda tume ya wanasheria wa kanisa mwaka jana kupiga msasa mbinu ya kurekebisha taratibu hizo zinazoruhusu wanandoa kuachana na kupunguza gharama .
Bila sheria hiyo wanandoa wa kikatoliki wanaotalikiana na kuolewa upya hutazamwa kama wazinifu na hawaruhusiwi kupokea komunio.
Mwandishi wa BBC mjini Vatican anasema kuwa Papa Francis hatabadilisha mafunzo ya katoliki kuhusu kuachana kwa wanandoa , lakini atawezesha kurahisisha wanandoa wenye matatizo kuthibitisha kuwa ndoa yao haikuwa ya maana tangu mwanzo
Mpango wa kutega mabomu watibuliwa Kenya
Wanaume watatu wamakamatwa mjini Nairobi nchini Kenya baada ya mtu mmoja kuzuiwa wakati anajaribu kuingia katika jengo la maduka akiwa na kifaa cha kilipuzi katika mkoba wake.
Kifaa hiko kiliharibiwa na polisi wa kitengo cha kutegua mabomu nchini kenya.
Shuhuda anasema watu hao watatu walisimamishwa na walinzi wa usalama wakiwa wanajaribu kuingia katika jengo moja la maduka la Garden city Mall kwenye kitongoji kimoja Nairobi.
Mmoja wa wanaume hao alikataa kukaguliwa hivyo ilibidi walinzi wamdhibiti wa kumpiga ngumi.
Milipuko iligunduliwa katika mkoba wake.
Wateja na wafanyakazi wa maduka hayo waliondolewa na kifaa hicho kiliharibiwa na kitengo maalum cha kudhibiti mabomu.
Polisi anasema wanaume wote watatu wanaoshukiwa kuwa ni raia wa Kenya wamekamatwa.
Inaaminiwa kuwa bomu hilo ni kilipuzi kidogo chenye betri na kilichounganishwa kwenye simu ya mkonon ambayo ingetumia kulipua bomu hilo.
Miaka miwili iliyopita watu 67 waliuawa baada ya wanamgambo wa Al Shabaab kuvamia maduka ya Wastegate mjini Nairobi.
Waandamanaji wafanya vurugu Uturuki
Maelfu ya waandamanaji waliokuwa wakipepea bendera za Uturuki wamevamia makao makuu ya chama kikuu cha Kikurdi cha HDP.
Jengo hilo lililoko katika mji mkuu wa Ankara baada ya kuvamiwa lilichomwa moto.
Chama hicho baadaye kilitoa maelezo kwamba majengo yake mengine yaliyoko kwenye miji mingine yalilengwa pia,mjini Kabul ambamo ziko ofisi za gazeti moja la Hurriyet zilishambuliwa kwa mara ya pili katika kipindi cha wiki mbili .
Naye waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu amelaani vikali mashambulizi na uvamizi huo katika ofisi za kisiasa na hata kwa nyumba za habari na ametoa wito wa kusitisha ghasia.
Mpaka sasa askari jeshi kumi na wanne wa Uturuji wanaarifiwa kupoteza maisha mapema wiki hii katika shambulio la bomu upande wa mashariki mwa nchi hiyo.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema majeshi yake yatapambana na magaidi wa nchi hiyo.
"Hatujaacha matarajio ya watu wetu na hatutaacha kwa magaidi, kwa makundi ya wanaotaka kuipindua nchi na washirika wao. Uturuki ambaye imewezakushinda mambo mengi hapo nyumba hadi sasa, itashughulikia suala la magaidi. Nchi yetu na wanajeshi wake, polisi na maafisa ujasusi wanajitahidi kupambana na makundi ya kigaidi nayogawa nchi pamoja silaha zao. Hadi sasa uharibufu mkubwa umefanywa na makundi hayo, kutoka ndani na nje ya mipaka yetu. matukio ya hivi sasa ni ya ziada, na kuchanganyikiwa kwa makundi hayo ni jambo tulilolizoea." amesema Erdogan.