Thursday, 11 December 2014

Ebola bado tishio Sierra Leone......















Maafisa wa Afya nchini Sierra Leone wamegundua miili kadhaa katika maeneo ya mgodi wa Almasi, na kusababisha hofu kuwa pengine ugonjwa wa Ebola haujaripotiwa ipasavyo.
Shirika la afya duniani,WHO limesema limebaini kisa hiki kipya mashariki mwa mji wa Kono, timu ya Wataalamu imepelekwa Kono kufanya uchunguzi kuhusu uwepo wa ugonjwa wa Ebola.
Watu 6,346 wamepoteza maish akutokana na ugonjwa huo na zaidi ya 17,800 wameathirika na Ebola.

Sierra Leone ina idadi kubwa zaidi ya Watu wenye Ebola Afrika Magharibi, ikiwa na Watu walioathirika 7,897 tangu kuanza kwa ugonjwa huo.
WHO imesema katika kipindi cha takriban siku 11 mjini Kono, Miili 87 ilizikwa.
Miili ya Watu waliokufa kutokana na maradhi ya Ebola ni hatari kwa maambukizi hivyo huzikwa kwa uangalifu mkubwa ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.
Share:

Mwanawe Rais Zuma hatiani Afrika Kusin....


Jopokazi moja nchini Afrika Kusini limesema kua mwanawe Jacob Zuma hakua makini alipokuwa anaendesha gari hadi kusababisha ajali ya barabarani ambapo mwanamke mmoja alifariki.
Awali kiongozi wa mashitaka hakuwa tayari kumchukulia hatua zozote za kisheria mwanawe Zuma. Sasa atakabiliwa na shinikizo za kumfungulia mashitaka.

Gari la Duduzane Zuma aina ya Porsche iligonga gari dogo la abiria mjini Johannesburg mwezi Februari, na kumuua mwanamke huyo papo hapo.
Mwandishi wa BBC Pumza Fihlani mjini Johannesburg anasema uamuzi huo unaonyesha uhuru wa vyombo vya sheria nchini humo.

Katika nchi ambapo swala la usawa bado ni tete, mahakama ndio mojawpao ya sehemu chache ambapo usawa unapatikana kwa wananchi na mwanawe Rais hajasazwa kwa hilo.
Rais Zuma ana watoto 21 na ameoa mara sita.

Duduzane mwenye umri wa miaka 30 aliambia jopokazi hilo kwa alipoteza mwelekeo wa barabaraalipokuwa anaendesha gari na kuingia ndani ya maji taka.
Hata hivyo hakimu alimwambia kwamba hakua na tabia njema hasa baada ya tukio hilo.
Mwezi Julai mamlaka ya mashitaka ilikataa kufungulia mashitaka kijana huyo ambaye pia ni mfanyabiashara na kosa la mauaji bila ya kukusudia ikisema hakuna ushahidi wa kutosha.
Share:

Punda watumiwa kutoa ujumbe Kenya......


Hii leo kulikuwa na taharuki katikati mwa mji wa Nairobi baada ya Punda waliokuwa wamepakwa rangi kupatikana wakizurura mjini humo.
Walikuwa na maandiko katika mwili wao yakisema: 'Tumechoka'
Neno 'Tumechoka' ni kauli mbiu ambayo ilitumiwa na mashirika ya kijamii kuelezea wasiwasi kuhusu hali ya utovu wa usalama nchini kote.

Kauli mbiu hio ilitumiwa mashambulizi yalipofanywa dhidi ya wakenya mjini Mandera Kaskazini mwa Kenya ambapo wanaharakati walipiga kambi katika ofisi ya Rais wiki kadhaa zilizopita kulalamikia ukosefu wa usalama.
Kwa kutumia Punda, kupitisha ujumbe wao, ni dhahiri kuwa ujumbe wao umefika kwa wengi.
Wanaharakati hao, wamewahi kutumia Nguruwe kuonyesha walivyo walafi na wafisadi wanasiasa wa Kenya.
Punda hao walikuwa 22 na walifikishwa kati kati ya mji kwa Lori. Dereva wa lori hilo alisema kuwa alilipwa na mtu flani kupeleka wanyama hao mjini.
Lori hilo lilipofikishwa mjini, mwanamume aliyekuwa amekodisha lori hilo aliamua kutoka kwenye Lori na wanyama hao.


Wanyama hao walinuiwa kutuma ujumbe kwamba wakenya wamechoshwa na hali mbaya ya usalama, alisema mwanaharakti mmoja aliyekuwa kwenye Lori hilo.
''Tumechoshwa na uongozi mbaya, '' alisikika akisema mwanaharakati mmoja huku akiwaskuma Punda hao kutoka kwa Lori.
Polisi wanasema wanawasaka wale waliohusika na kitendo hicho.
Share:

Baiskeli iliyotengezwa kwa dhahabu...........


Ni rahisi sana kwa watu kulalamikia gharama ya kununua baiskeli wengi wakitaka bei nafuu. Nyingi ya baiskeli nchini Uingereza huuzwa kwa pauni 1,000 shilingi lakini moja na arobaini pesa za Kenya.
Kwa wengi nchini humo hizo ni pesa nyingi sana.
Hata hivyo baikeli mpya iliyotengezwa kwa dhahabu imezinduliwa nchini humo. Bei yake? Pauni laki mbili na hamsini au milioni 36,250,000 pesa za kenya. Bei hii ni ghali hata kuliko bei ya gari jipya la Ferari, kukufahamisha tu.















Baiskeli hio ambayo ilitengezwa na kampuni ambayo hutengeza vitu vya kifahari, Goldgenie imetengezwa kwa dhahabu kutoka kwa mikono na vyuma vyake vyote. Kiwango cha dhahabu iliyotumiwa ni karati 24.
Wataalamu wa kampuni hio ya Goldgenie, wameweka dhahabu katika vyuma vya baiskeli hio vyote , mnyororo na mfumo unaofanya baiskeli kwenda na kubadilisha gia vyote vimewekwa dhahabu.
















Na wakati baiskeli hio inavutia macho, inapowekwa nyuma ya kabati ya glasi na kulindwa na walinzi. Mkrugenzi wa kampuni hio anasema baiskeli hio inaweza kuendeshwa kwenye barabara.
"baiskeli hii sio tu ya kuvutia macho, bali pia ni nzuri ya kuendesha ikiwa mwenye kuiendesha atsatahimili kuangaliwa sana.''
Muundo wa baiskeli hii ni wa hali ya juu,'' aliongeza kusema mkurugenzi huyo.
Kwa sasa haijulikani idadi ya baiskeli hizo zitakazotengezwa, lakini ikiwa utakuwa na bahati sana unweza kupata moja kama hio. Lakini itakubidi ununue kufuli kuifungia baiskeli yako ikiwa hautakuwepo ambako umeiwacha.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.