Rais
Jose Mujika na mkewe ndani ya gari lao la Vokswagen
Bwana
Mujica ,aliyejulikana kama rais masikini duniani kutokana na maisha
yake, alisema kuwa ombi hilo lilitoka kwa kiongozi mmoja wa dini ya
kiislamu katika eneo la uarabuni.
Aliliambia
gazeti la kila wiki la Busqueda kwamba iwapo atalikubali ombi hilo
basi fedha hizo zitatumiwa kuwasaidia masikini.
Rais
Mujika ambaye anajulikana kama Pepe anaishi katika shamba lake na
hutoa pato lake kwa watu masikini.
Mnamo
mwaka 2010 Mali yake ilikuwa inagharimu dola 1,800 ambayo ni bei ya
gari lake la Volkswagen
Busqueda
liliripoti kwamba ombi la gari hilo lilifanywa katika mkutano wa
kimataifa mapema mwaka huu katika mji wa Santa Cruz Bolivia.
''Nilishangaa
mara ya kwanza ,a hivyobasi nikapuzilia mbali.lakini baadaye ombi
jengine lilikuja na hivyobasi nikaanza kulichukulia kuwa swala la
umuhimu'',. Alisema Mujika.