Menu - Pages

Saturday, 8 November 2014

Rais wa Uruguay Jose Mujika anasema kuwa amepewa dola millioni 1 ili kuuza gari lake aina ya Volkswagen...... BBC

Rais Jose Mujika na mkewe ndani ya gari lao la Vokswagen
Bwana Mujica ,aliyejulikana kama rais masikini duniani kutokana na maisha yake, alisema kuwa ombi hilo lilitoka kwa kiongozi mmoja wa dini ya kiislamu katika eneo la uarabuni.
Aliliambia gazeti la kila wiki la Busqueda kwamba iwapo atalikubali ombi hilo basi fedha hizo zitatumiwa kuwasaidia masikini.
Rais Mujika ambaye anajulikana kama Pepe anaishi katika shamba lake na hutoa pato lake kwa watu masikini.
Mnamo mwaka 2010 Mali yake ilikuwa inagharimu dola 1,800 ambayo ni bei ya gari lake la Volkswagen
Busqueda liliripoti kwamba ombi la gari hilo lilifanywa katika mkutano wa kimataifa mapema mwaka huu katika mji wa Santa Cruz Bolivia.

''Nilishangaa mara ya kwanza ,a hivyobasi nikapuzilia mbali.lakini baadaye ombi jengine lilikuja na hivyobasi nikaanza kulichukulia kuwa swala la umuhimu'',. Alisema Mujika.

Visa vya Ebola vyapungua Liberia

Shirika la madaktari wasio na mipaka Medecins Sans Frontieres limesema kuwa viwango vya Ebola nchini Liberia humo vimeshuka kidogo.
Hata hivyo shirika hilo limeonya kuwa kuna ongezeko la visa vya ugonjwa huo nchini Guinea na Sierra Leone likisema kuwa visa vya maambukizi vilivyokuwa vimepungua nchini Guinea vimeongezeka tena.
Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa mafanikio nchini Liberia yanatokana na jitihada za kuzika maiti kwa njia iliyo salama.

WHO inasema kuwa karibu watu 5000 wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo

USA:Mwanamke mweusi (Loretta Lynch)ateuliwa kuwa mwanasheria mkuu wa marekani...... BBC

Ikulu ya white house nchini Marekani inasema kuwa rais Barack Obama amemteua mwendesha mashtaka wa mji wa New York Loretta Lynch kuwa mkuu wa sheria nchini humo. Msemaji wa ikulu ya white house alisema kuwa mkuu huyo mpya wa sheria atateuliwa rasmi leo Jumamosi. Ikiwa uteuzi wake utaidhinishwa na bunge la seneti Loretta Lynch atakuwa mwanamke wa kwanza mwenye asili ya afrika kuwa mkuu wa sheria nchini marekani . Uteuzi huo unafanyika wiki sita baada ya kujiuzulu kwa Eric Holder ambaye ndiye M'marekani wa kwanza mweusi kuteuliwa kuwa mkuu wa sheria nchini humo.

Miaka mia moja iliyopita, kilikuwa chombo kilichokuwa kinatisha na kutawala katika Ziwa Tanganyika.


Hii leo, chombo hiki ni moja ya meli za zamani kabisa duniani zinazobeba abiria. Chombo hicho, kilichopewa jina la The Goetzen, kilipelekwa Afrika Mashariki, kusaidia kulinda koloni la Ujerumani wakati huo, dhidi ya majeshi ya ushirika, wakati wa Vita kuu ya kwanza ya dunia.