Tuesday, 9 December 2014

Al Jazeera yaihusisha Kenya na mauaji.....source BBC


Shirika la habari la Al Jazeera limepeperusha ripoti ambayo imehusisha maafisa wa usalama wa Kenya na mauaji ya viongozi wa dini ya kiisilamu pamoja na washukiwa wa ugaidi.
Taarifa hiyo ya ufichuzi iliyopeperushwa Jumatatu, ilionyesha baadhi ya maafisa wa polisi wanaofanya kazi yao kwa usiri mkubwa wakikiri kuwaua baadhi ya viongozi wa kiisilamu wanaosemekana kufunza mafunzo yenye itikadi kali ya kiisilamu pwani ya Kenya.

Ripoti hio http://goo.gl/wYV91g ambayo ilikuwa ni kanda ya video yenye polisi hao wakikiri kuwaua waisilamu mjini Mombasa, iliwekwa kwenye mtandao wa YouTube na shirika hilo.
Inaonyesha sura za polisi hao zikiwa zimefichwa huku wakisimulia ambavyo wamekuwa wakiwaua watu wanaonekana kua wenye kutoa mafunzo ya itikadi kali na wanaotatiza usalama wa nchi.
Wengi ambao wameuawa na maafisa hao ni washukiwa wa ugaidi waliodaiwa kutoa mafunzo ya itikadi kali za kidini.

Walisema kuwa wampokea mafunzo yao kutoka kwa mashirika ya kijasusi ya kimataifa ikiwemo MI5 la Uingereza na Mossad la Israel.
Mmoja wa maafisa anasema wamewaua washukiwa wengi sana wa ugaidi akiwemo Sheikh Abubakar Shariff Makaburi mnamo mwezi April.
Taarifa hizo zilichapishwa kwenye vyombo vingine vya habari vikizungumzia mauaji ya kisiri ya washukiwa wa Ugaidi yanayofanywa na maafisa wa polisi waliopata mafunzo ya hali ya juu nchini Kenya.

Baadhi ya maafisa hawa wanatoka kitengo cha polisi wa kupambana na ghasia au GSU na shirika la kitaifa la ujasusi.
Mmoja wao alinukuliwa akisema katika kanda hio ....''sisi hupewa taarifa tu na kisha kutekeleza matakwa ya wakuu wetu. Huwa tunamuua yule mshukiwa tuliyetumwa kumuu na kazi hii huwa tunaifanya kwa usiri mkubwa sana,''

wote waliohojiwa wanasema wao hupokea mafunzo ya hali ya juu mno kabla ya kufanya kazi yao kwa umakini mkubwa.
Ripoti hiyo ya Al Jazeera inasema kuwa washukiwa wa ugaidi huuawa badala ya kupelekwa mahakamani.

Sio mara ya kwanza kwa mashirika ya usalama nchini Kenya kutuhumiwa kwa mauaji ya washukiwa wa ugaidi kwa siri.
Hata hivyo, Serikali ya Kenya imetoa taarifa kupinga ripoti hio inayodai kuwa polisi nchini humo walihusika na mauaji ya washukiwa wa ugaidi.

Ripoti hiyo iliyoonyeshwa na runinga ya al jazeera ilidai kuwa maafisa kadhaa wa polisi walikiri kuwa kikosi maalum cha usakama kilihusika na kutoweka na hatimaye mauaji wa washukiwa wa ugaidi, hasa viongozi wa dini ya kiislamu waliokiswa kuwa na siasa za misimamo mikali.
Lakini katibu wa wizara ya habari nchini Kenya amesema ripoti hiyo haina msingi wowote na kutaka shirika hilo la habari kuiomba msamaha.
Share:

Watoto wa kiume Culcutta sio dili.........

Polisi Mashariki mwa mji wa Calcutta nchini India, wanachunguza tukio la mwanamke ambaye jamii yake ilimtelekeza katika bwawa,kwa kushindwa kuzaa mtoto wa kike ambaye baadaye walimtegemea kuwa kahaba.

Mwanamke huyo aliokolewa na chama cha kujitolea kuwahudumia makahaba kabla hajalazimika kujitosa kwenye ukahaba kamili.
Mwanamke huyo aliiambia BBC kwamba familia ya wakwe zake walianza kumdhihaki baada ya kuzaa watoto wa kiume watatu mfululizo, na kufahamishwa kwamba familia hiyo kwa kawaida huwapeleka watoto wa kike wa ukoo wao kufanya kazi ya ukahaba, iweje yeye azae watoto wakiume watupu?.
Share:

Rais Mugabe amfuta kazi makamu wake....


Taarifa kutoka nchini Zimbabwe zinasema kuwa Rais Robert Mugabe amemfuta kazi makamu wake Joice Mujuru, kufuatia ushindani wa uongozi katika chama tawala cha ZANU-PF.
Awali Bi Joyce Mujuru, alikanusha madai kuwa yeye ni mfisadi na alihusika na njama ya kutaka kumuua rais Robert Mugabe.

Bi Mujuru alilaaniwa na Rais Mugabe wiki iliyopita na kuondolewa kutoka wadhifa wake wa makamu wa rais wa chama tawala cha ZANU-PF wakati wa kongamano la chama hicho mjini Harare.

Amesema ameendelea kupokea vitisho na kuwa shirika la habari la serikali limeendelea kuchapisha habari za uongo za zisizo na msingi dhidi yake.
Ilikuwa wiki nzima ya tuhuma dhidi ya Bi Mujuru kutoka kwa vyombo vya habari vya serikali kwa ushirikiano na mkewe Mugabe, Grace Mugabe, ambaye kwa sasa ameteuliwa kama afisaa mkuu wa chama cha ZANU-PF.

Wengi walimuona Mujuru mwenye umri wa miaka 59, kama mrithi wa Mugabe.
Katika hatua yake ya kwanza kujibu tuhuma hizo tangu kuondolewa katika chama, Mujuru alisema amekuwa akitishiwa sana na watu asio wajua.
Aliongeza kuwa vyombo vya habari nchini humo vimeendelea kumchafulia jina lake kwa kuchapisha porojo na taarifa za uongo, dhidi yake.
Alisema hakuna hjata tone moja la ushahidi limetolewa dhidi yake kuthibitisha madai anayasingiziwa na kutajwa kuwa msaliti mkubwa.

Madai kuwa alipanga njama ya kumuondoa mamlakani Mugabe, ni ya kipuzi sana.
Rais Mugabe, mwnye umri wa miaka 90, amekua mamlakani tangu Zimbabwe kujipatia uhuru mwaka 1980.
Bi Mujuru alipambana bega kwa bega na Mugabe mapema miaka ya 1970, dhidi ya utawala wa kibaguzi na kwa wengi alionekana kama mrithi mtarajiwa wa Mugabe.
Share:

Askofu Desmond Tutu ana tezi dume....


Askofu mkuu mstaafu wa Cape Town,Desmond Tutu,ameahirisha mipango ya ziara zake kwa mwaka mzima ujao kutokana na sababu za kiafya.

Taarifa iliyotolewa na taasisi yake imeeleza kuwa Askofu huyo ataanza matibabu hivi karibuni ili kukabiliana na tezi dume ambayo amedumu nayo miaka kumi na mitano iliyopita.
Binti wa Askofu huyo amemuelezea baba yake mwenye umri wa miaka themanini na miwili,kwamba hatahudhuria tuzo za Nobel zitakazo fanyika baadaye wiki hii huko Rome, Italia.
Share:

Daktari feki akamatwa Tanzania.......












Hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam, Tanzania


Sekta ya afya nchini Tanzania bado inakabiliwa na tatizo la madaktari feki ambapo jana Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu, MOI ilimkamata daktari feki aliyefahamika kwa jina la Dismas John Macha mwenye umri wa miaka 35.

Taasisi hiyo ipo kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, MNH jijini Dar es Salaam, ambapo daktari huyo anadaiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa wagonjwa na ndugu wa wagonjwa kwa madai kwamba angemhudumia mgonjwa wao.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, Mkurugenzi wa MOI, Athumani Kiloloma, alisema mara ya kwanza alikamatwa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, MUHAS, akijifanya mwanafunzi wa shahada ya uzamili katika shule ya tiba.
Dk. Kiloloma alisema alipokamatwa mara ya kwanza, walitoa matangazo katika hospitali nzima na kutoa taarifa kwa wananchi, lakini wanashangaa tukio hilo limejirudia tena.
Akizungumzia tukio hilo, mkurugenzi huyo alisema wanakabiliwa na tatizo kubwa la madaktari feki, ambao wamekuwa wakiomba michango mbalimbali ya fedha.

Mtuhumiwa Dismas Macha anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayomkabili.
Awali, Dismas akizungumza na waandishi wa habari, alisema yeye si daktari bali ni mgonjwa wa akili. Matukio ya madaktari feki yamekuwa yakiripotiwa katika hospitali mbalimbali nchini Tanzania katika siku za karibuni, ambapo inadaiwa madaktari hao kazi kubwa ni kuwatapeli wagonjwa na ndugu wa wagonjwa.
Share:

Watanzania waadhimisha miaka 53 ya uhuru..........


Tanzania bara leo inaadhimisha miaka 53 toka ilipojipatia uhuru toka kwa Muingereza Desemba 9, mwaka 1961.
Maadhimisho haya ya 53 ni muhimu kwa Watanzania, kutokana na kwamba nchi ipo katika kipindi cha uchaguzi, ambapo Watanzania siku ya Jumapili Desemba 14, watapiga kura, katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji.
Uchaguzi huo ni muhimu, kutokana na viongozi katika ngazi hiyo kuwa karibu kabisa na jamii.
Tanzania pia inaadhimisha miaka 53 ya uhuru wake ikiwa katika harakati za uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Ni miaka 53 tangu Tanzania ijipatie uhuru wake, lakini hali za Watanzania wengi bado ni duni, kiuchumi na kijamii.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.