Rais
Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema kuwa Kenya haitachoka katika vita
vyake dhidi ya ugaidi kufuatia shambulizi lililofanywa dhidi ya
wachimba migodi mjini Mandera Kaskazini ya Kenya.
Ametoa
kauli hiyo katika hotuba yake kwa taifa baada ya shambulizi lengine
lililofanywa na kundi la wanamgambo la Al Shabaab dhidi ya wakenya
wasiokuwa na hatia.
Kundi
hilo liliwavamia wachimba migodi 36 waliokuwa katika machimbo ya
kokoto mjini Mandera.
Kundi
hilo liliwaua wakenya wengine 28 waliokuwa wanasafiri kutoka mjini
Mandera siku kumi zilizopita.
Kenyatta
amelaani wanamgambo hao wa Al Shabaab kwa kutaka kuigawanya Kenya
katika msingi ya kidini na kuwataka wakenya kuungana dhidi ya kile
alichokitaja vita dhidi ya ugaidi.
Kenyatta
aliwataka magaidi wa Al Shabaab kama wanyama walio na kichaa.
Aliwasihi
wakenya kuungana katika vita dhidi ya magaidi.
Siku
kumi zilizopita, Al Shabaab waliuwaua abiria 28 waliokuwa wanasafiri
kwa basi kutoka mjini Mandera karibu na mpaka na Somalia kuelekea
likizoni makwao. Wengi wa waliouawa walikuwa walimu wa shukle za
umma.
0 comments:
Post a Comment