Polisi mjini Mombasa wamewakamata watu 15 kuhusiana na mauaji ya watu wanne usiku wa kuamkia leo mjini humo.
Lakini
wamekanusha kuwa mauaji hayo yalihusishwa na msako wa polisi dhidi ya
misikiti inayotoa mafunzo ya itikadi kali mjini humo. Hali ya taharuki bado iko juu katika baadhi ya maeneo mjini humo huku polisi wakiendelea kushika doria mjini humo.
Kamishna mkuu wa Mombasa, Nelson Marwa anasema kuwa wale wote waliohusishwa na mauaji hayo ya watu wanne kwa kuwadunga visu, walikodiwa na mwanasiasa katika mtaa wa Kisauni.
Marwa hata hivyo amesema idadi ya wale waliouawa sio watu wanne bali ni watatu.
Hata hivyo jamaa wa waliouawa walithibitisha idadi yao kuwa watu wanne ambao walifariki baada ya kudungwa visu.
Wengine zaidi ya 12 walijeruhiwa kwenye tukio hilo ambalo limejhusishwa na vijana wenye itikadi kali za kidini.
Zaidi ya vijana 250 walikamatwa baada ya kupatikana na maguruneti pamoja na silaha nyinginezo kwenye msako uliofanywa Jumatatu asubuhi.
Viongozi wa kiisilamu na mashirika mengine ya kutetea haki za binadamu wamelaani msako huo ambao wanasema utarejesha tu hisia za waisilamu kulengwa na maafisa usalama.
No comments:
Post a Comment