Shahidi mmoja muhimu wa uchunguzi
unaofanyika kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda ambaye alikuwa
akitarajiwa kuhojiwa na majaji Nchini Ufaransa kuhusu kudunguliwa kwa
ndege ya aliyekuwa rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana, anasemekana
kutekwa nyara na kutoweka jijini Nairobi.
Idara ya Polisi Nchini Kenya imekanusha kumtia mbaroni Emile Gafirita.Majirani wa Emile Gafirita wanasema kuwa walisikia milio ya breki za gari na kamsa pale alipokuwa akirejea nyumbani muda mfupi kabla ya usiku wa manane Jumatatu usiku na kuwaona watu wawili wakimtia pingu na kumrusha kwenye gari.
Idara ya Polisi Nchini Kenya inasema kuwa hawajamtia mbaroni.
Jina la bwana Gafirita liliibuka katika kesi ya hivi majuzi Nchini Rwada, pale alipotajwa kama askari wa zamani katika kikosi cha ulinzi cha Rais Paul Kagame.
Majaji wawili wa Ufaransa, Marc Trevidic na Nathalie Poux, walikuwa wakipanga kumhoji ili atoe ushahidi mjini Paris kuhusiana na mzinga ulioshambulia na hatimaye kuiangusha ndege iliyombeba Rais wa zamani wa Rwanda hayati Juvenal Habyarimana mnamo mwezi Aprili ya mwaka 1994.
Mauaji ya Habyarimana yaliibua mapigano makali ya kikabila yaliyosababisha mauwaji ya zaidi ya watu laki nane, wengi wao waTusti na wahutu wenye siasa za kadri.
No comments:
Post a Comment