Monique
akiwa mbele ya TV akiomba binti yake kurejea nyumbani Uholanzi miezi
miwili iliyopita
Msichana wa kiholanzi aliyerejea kutoka Syria ambako
alikwenda huko kujiunga na wapiganaji wa jihadi lakini baadaye
alirudishwa nyumbani na mamake anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa
kushukiwa kutishia usalama wa taifa.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 19, akijulikana kama
Aicha, alikamatwa aliporejea nyumbani kwao katika mji wa Maastricht.
Aicha, aliyebadili dini hivi karibuni kuwa Mwislam,
anaaminika kusafiri kwenda kujiunga na wapiganaji wa Islamic State
(IS) katika ngome ya Raqqa nchini Syria kuoana na mpiganaji mmoja.
Mama yake Monique alisaidia kumrejesha nyumbani Uholanzi
na si mtuhumiwa.
Aicha ni mmoja wa idadi ndogo ya wasichana na wanawake
kutoka Ulaya ambao wamekwenda Syria na Iraq katika miezi ya karibuni.
Baadhi wanaaminika kusafiri kwenda hukokupata mafunzo ya
kiitikadi, wakati wengine wanasemekana kuoana na wapiganaji, wakiwemo
wanaopigana bega kwa bega na wapiganaji wa IS.
Mahakama nchini Uholanzi Ijumaa itasikiliza kesi hiyo
bila wasikilizaji na itaamliwa Aicha anaweza kushikiliwa kwa muda
gani.
Upande wa mashitaka unatarajiwa kumwomba jaji kuongeza
muda wa kumshikilia Aicha wakati wakichunguza ushahidi.
No comments:
Post a Comment