Rais
Barack Obama amelihotubia taifa kueleza mageuzi makubwa katika mfumo
wa uhamiaji wa Marekani. Amesema atachukua hatua za kikatiba kutoa
ruhusa ya muda kisheria kwa takriban wahamiaji haramu milioni tano.
Obama amesema nchi hiyo ilijengwa kwa uhamiaji na ameshutumu
wanachama wa Republican kwa kuzuia mageuzi hayo. Wanachama hao
wametishia kuchukua hatua.
Amesema
watakaohalalishwa watalazimika kulipa kodi na wasiwe na rekodi ya
uhalifu. Hata hivyo amesema urejeshwaji makwao kwa watu wenye makosa
utaharakishwa.
Bwana
Obama ametangaza mpango wake, ambao anaupitisha bila baraza la
Congress, katika hotuba aliyoitoa kupitia televisheni.
Kwa
upande wao wajumbe wa Republican wamesema hatua ya Rais Obama inavuka
mipaka yake na uhusiano na rais utaingia dosari
Kuna
wahamiaji wasio halali wapatao milioni 11 nchini Marekani na mwaka
huu watoto wanaovuka mpaka wamesababisha tatizo.
Rais
Obama ameliambia taifa kuwa kile anachopendekeza sio msamaha
"Ninachokieleza
ni uwajibikaji - akili ya kawaida, mtazamo wa kawaida," amesema.
"Kama
unatimiza vigezo, unaweza kujitokeza na kuishi maisha ya kawaida
ukiendana na sheria."
"Iwapo
ni mhalifu utarejeshwa ulikotoka.Kama unapanga kuingia Marekani
kinyume cha sheria, nafasi ya kukamatwa na kurejeshwa ulikotoka ni
kubwa." anasema Rais Obama.
Rais
Obama amesema mfumo mpya wa uhamiaji utawawezesha watu wanaoishi
nchini Marekani kinyume cha sheria, kujulikana na kuchangia katika
uchumi wa taifa kwa kuwa watakuwa huru kufanyakazi.
Kuamuru
kufanyika kwa mageuzi hayo kumesababisha malalamiko ya hasira kwa
wanachama wa Republicans ambao wanasema hatua hiyo ni
kutolishirikisha baraza la Congress na kuendesha mambo kwa mfumo wa
Kifalme. Baadhi wanasema hawatatoa ushirikiano katika maeneo mengine
ya kisera, na wengine wamemtaka Bwana Obama ashitakiwe.
Rais
Obama anasema anachukua hatua hiyo kwa sababu baraza la Congress mara
kadha kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu limeshindwa kurekebisha mfumo
wa uhamiaji ambao umeharibika.
No comments:
Post a Comment