Menu - Pages
▼
Friday, 21 November 2014
Basi linalotumia kinyesi lazinduliwa.......
Basi la kwanza nchini Uingereza linalotumia kinyesi na uchafu unaotokana na chakula limeanza safari yake ya kwanza>>>>>INGIA HAPA<<<<<
wanawake
wakiandamana huku wakiomboleza nchini Uganda
shughuli
za mazishi ya mtoto wa miaka miwili zimefanyika nchini Uganda, mtoto
ambaye kifo chake kimezua ghadhabu baada ya mtoto huyo kugongwa na
gari la halmashauri ya jiji la Kampala ,baada ya mama yake kukamatwa
akiuza matunda kinyume cha sheria.
Familia
ya Ryan Ssemaganda na wanasiasa wa upinzani walitishia kutomzika
mtoto huyo mpaka maofisa hao watakapo wajibika kwa kitendo
hicho.Mwili wake ulichukuliwa wakati wakiandamana kuelekea bungeni
siku ya alhamisi.
Raia
wa Uganda wanaona kuwa halmashauri hiyo inatumia nguvu nyingi
kupambana na wachuuzi wa mitaani.
Mama
wa mtoto Ryan alikamatwa siku ya jumatatu baada ya kukutwa akiuza
matunda huku akiwa hana leseni.
Siku
iliyofuata, Bibi wa mtoto huyo alimpeleka katika Ofisi za Mamlaka ya
mji wa Kampala ambako mama mtoto alikuwa akishiliwa , nia ilikua
kumpa mama mtoto ili amnyonyeshe.
Maafisa
wa Ofisi hiyo walikataa na wakati wakijadiliana kuhusu hilo, mtoto
alichoropoka kutoka kwa mama yake na kugongwa na gari linalomilikiwa
na Mamlaka hiyo.
Siku
ya Alhamisi polisi ilizuia kupelekwa kwa mwili katika Bunge,
wakisisitiza mwili huo uzikwe ili marehemu apumzike kwa amani, na
kuwataka waepuka jambo hilo kushughulikiwa kisiasa.
Mkanyagano hatari wawaua 11 Zimbabwe.......
Watu
11 wamefariki katika mkanyagano nchini Zimbabwe baada ya ibada ya
kidini kufnayika katika uwanja wa soka.
Polisi
wanasema kuwa watu wanne walifariki katika uwanja huo ulio mjini
Kwekwe wakati wengine saba wakifariki hospitalini.
Mkanyagano
huo ulitokea wakati maelfu ya waumini wakikimbilia kuondoka uwanjani
humo baada ya ibada iliyoongozwa na mhubiri wa kipentekoste Walter
Magaya.
Mhubiri
huyo anadai kuwaponya watu kwa kufanya miujiza.
Baadhi
ya walioshuhudia mkanyagano huo wanatuhumu polisi kwa kufunga baadhi
ya milngo ya kuondokea uwanjani humo, huku watu wakiondoka kupitia
mlango mmoja tu.
Hata
hivyo polisi wanakana kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya.
Bwana
Mugaya ambaye ni mkuu wa kanisa la 'Prophetic Healing and
Deliverance' aliambia vyombo vya habari kuwa alipopata habari ya
kutokea vifo hivyo alihuzunika sana.
Shambulio laua tena Mombasa Kenya.....source BBC
Mtu
mmoja ameripotiwa kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mapigano
katika mji wa Mombasa pwani ya Kenya. Polisi walipambana na vijana
walioingia katika Msikiti wa Swafaa eneo la Kisauni na mpaka sasa
zaidi ya vijana 400 wanashikiliwa tangu kuanza kwa msako huo, mapema
wiki hii.
Mwandishi wa BBC, Emmanuel Igunza anasema Msikiti huo
ulifungwa jana baada ya polisi kuuvamia Jumatano, ambamo walipata
magruneti, mabomu ya petroli na silaha nyingine. Hali ya wasi wasi
bado imetanda katika mji huo wa pwani. Serikali imekwishafunga
misikiti minne ambayo wanasema ina uhusiano wa watu wenye misimamo
mikali ya imani ya kidini.
Pamoja na kukamata silaha
mbalimbali, polisi pia walikamata bendera nyeusi, alama ya kuunga
mkono kundi la kigaidi la Al-Shabab la nchini Somalia
Awali polisi mjini Mombasa pwani ya Kenya walisema
wamepata silaha nyingine zaidi yakiwemo mabomu katika msikiti wa tatu
ambao ulifanyiwa upekuzi Msako huo katika msikiti wa Swafaa mtaani Kisauni
unakuja baada ya msako mwingine wa Jumatatu ambapo polisi pia
walipata silaha ndani ya msikiti ambao wanasema hutumika kutoa
mafunzo yenye itikadi kali.
Mtaa wa Kisauni ndiko vijana waliokuwa wamejihami
kuwadunga visu watu wanne na kuwaua. Pia waliwashambulia kwa silaha
nyingine.
Waziri wa usalama wa ndani, Joseph Ole Lenku anasema
kuwa msako huo ulifanywa katika misikiti ambayo hutumiwa na watu
wanaoeneza itikadi kali za kiisilamu kwa vijana ambao inadaiwa
wanajiunga na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab nchini
Somalia.
Viongozi wa kiisilamu wamelaani misako hiyo katika
Misikiti wakisema kuwa itachochea zaidi vijana kuendeleza itikadi
kali za kidini.
Rais Obama awatangazia neema wahamiaji.....source BBC
Rais
Barack Obama amelihotubia taifa kueleza mageuzi makubwa katika mfumo
wa uhamiaji wa Marekani. Amesema atachukua hatua za kikatiba kutoa
ruhusa ya muda kisheria kwa takriban wahamiaji haramu milioni tano.
Obama amesema nchi hiyo ilijengwa kwa uhamiaji na ameshutumu
wanachama wa Republican kwa kuzuia mageuzi hayo. Wanachama hao
wametishia kuchukua hatua.
Amesema
watakaohalalishwa watalazimika kulipa kodi na wasiwe na rekodi ya
uhalifu. Hata hivyo amesema urejeshwaji makwao kwa watu wenye makosa
utaharakishwa.
Bwana
Obama ametangaza mpango wake, ambao anaupitisha bila baraza la
Congress, katika hotuba aliyoitoa kupitia televisheni.
Kwa
upande wao wajumbe wa Republican wamesema hatua ya Rais Obama inavuka
mipaka yake na uhusiano na rais utaingia dosari
Kuna
wahamiaji wasio halali wapatao milioni 11 nchini Marekani na mwaka
huu watoto wanaovuka mpaka wamesababisha tatizo.
Rais
Obama ameliambia taifa kuwa kile anachopendekeza sio msamaha
"Ninachokieleza
ni uwajibikaji - akili ya kawaida, mtazamo wa kawaida," amesema.
"Kama
unatimiza vigezo, unaweza kujitokeza na kuishi maisha ya kawaida
ukiendana na sheria."
"Iwapo
ni mhalifu utarejeshwa ulikotoka.Kama unapanga kuingia Marekani
kinyume cha sheria, nafasi ya kukamatwa na kurejeshwa ulikotoka ni
kubwa." anasema Rais Obama.
Rais
Obama amesema mfumo mpya wa uhamiaji utawawezesha watu wanaoishi
nchini Marekani kinyume cha sheria, kujulikana na kuchangia katika
uchumi wa taifa kwa kuwa watakuwa huru kufanyakazi.
Kuamuru
kufanyika kwa mageuzi hayo kumesababisha malalamiko ya hasira kwa
wanachama wa Republicans ambao wanasema hatua hiyo ni
kutolishirikisha baraza la Congress na kuendesha mambo kwa mfumo wa
Kifalme. Baadhi wanasema hawatatoa ushirikiano katika maeneo mengine
ya kisera, na wengine wamemtaka Bwana Obama ashitakiwe.
Rais
Obama anasema anachukua hatua hiyo kwa sababu baraza la Congress mara
kadha kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu limeshindwa kurekebisha mfumo
wa uhamiaji ambao umeharibika.
Msichana kutoka Syria ashitakiwa.....
Monique
akiwa mbele ya TV akiomba binti yake kurejea nyumbani Uholanzi miezi
miwili iliyopita
Msichana wa kiholanzi aliyerejea kutoka Syria ambako
alikwenda huko kujiunga na wapiganaji wa jihadi lakini baadaye
alirudishwa nyumbani na mamake anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa
kushukiwa kutishia usalama wa taifa.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 19, akijulikana kama
Aicha, alikamatwa aliporejea nyumbani kwao katika mji wa Maastricht.
Aicha, aliyebadili dini hivi karibuni kuwa Mwislam,
anaaminika kusafiri kwenda kujiunga na wapiganaji wa Islamic State
(IS) katika ngome ya Raqqa nchini Syria kuoana na mpiganaji mmoja.
Mama yake Monique alisaidia kumrejesha nyumbani Uholanzi
na si mtuhumiwa.
Aicha ni mmoja wa idadi ndogo ya wasichana na wanawake
kutoka Ulaya ambao wamekwenda Syria na Iraq katika miezi ya karibuni.
Baadhi wanaaminika kusafiri kwenda hukokupata mafunzo ya
kiitikadi, wakati wengine wanasemekana kuoana na wapiganaji, wakiwemo
wanaopigana bega kwa bega na wapiganaji wa IS.
Mahakama nchini Uholanzi Ijumaa itasikiliza kesi hiyo
bila wasikilizaji na itaamliwa Aicha anaweza kushikiliwa kwa muda
gani.
Upande wa mashitaka unatarajiwa kumwomba jaji kuongeza
muda wa kumshikilia Aicha wakati wakichunguza ushahidi.