Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka.
Mheshimiwa
Bi. Anna Tibaijuka (Mb), Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi ni moja wa viongozi wachache sana wenye ujasiri na kiongozi
muwazi katika sakata zima la akaunti ya Tageta Escrow, kwani kiongozi
huyu amekiri wazi kuwa amepokea fedha shilingi billion 1.6 kutoka kwa
mmiliki wa kampuni ya VIP Engineering Bw. James Rugimalira.
Si
jambo jema kumhukumu Mheshimiwa Anna Tibaijuka, lakini siyo vibaya
kumshauri kwa kuwa amekuwa muwazi katika sakata hili, basi lingekuwa
jambo la maana sana kama angejiuzulu madaraka aliyonayo katika
serikali ili kulinda heshima yake na ya chama tawala.
Msomi
yoyote yule anapofikia kuitwa Profesa na tena Waziri mwenye kushika
dhamana ya nchi na wananchi yaani, Ardhi na Makazi, halafu akakubali
kupokea fedha ya kiasi kikubwa hivyo bila ya kutia shaka yoyote kama
ananuliwa kwa namna moja au nyingine kutokana na dhamana ya cheo
chake, litakuwa ni jambo jema kwake kujiuzulu ili aonyeshe mfano bora
kuwa yeye ni kiongozi mkweli na viongozi wengine wafuate nyao.
Msomi
aliyefikia daraja la juu kabisa tunamwona kama kiongozi anayejua wazi
kuwa yeye ni mojawapo wa Mawaziri wachache ambao Wizara zao zina
dhamana kubwa ya nchi, leo hii akikubali kununuliwa kiurahisi au
kufanya biashara akiwa katika madaraka mazito, tuna mashaka naye
ikiwa atandelea kututumikia wananchi katika Wizara ambayo pia
inahusika na mipaka ya ardhi ya nchi.
Watanzania
tunajiuliza, hivi Mhe. Anna Tibaijuka yupo katika utumishi wa umma
tena na huku akiwa Mkurugenzi wa Mashirika au Shule na miradi
binafsi, ndiyo kusema cheo chake cha utumishi wa umma ndio dhamana ya
biashara zake?
Hivi
kuna hosptali ngapi hapa nchini hazina dawa? Je wakina mama wangapi
wajawazito wanafariki wakati wa kujifungua kwa ukosefu wa vifaa vya
mahosptalini? Shule ngapi za serikali hazina madawati?
Leo
Mheshimiwa mabilioni ya fedha na kusema kuwa hakujua kama ni fedha
chafu. Kwa vipi Watanzania tusiwe na mashaka naye?
Professor
Anna Tibaijuka anafahamu wazi kuwa amevunja sheria ya maadili ya
viongozi wa umma "(Sheria namba 13 ya mwaka 1995) ambayo
inawataka viongozi watoe taarifa ya zawadi wanazopokea au malipo
wanayolipwa."
Hivyo,
sisi wananchi wenye kuiamini serikali hii hautuwezi kabisa kukubali
au kuona kiongozi tena msomi anavunja dhamana ya wananchi na
kumvunjia heshima mkuu wa nchi ambaye ndiye alimteua.
Litakuwa
jambo la busara sana Mhe. Anna Tibaijuka ujiuzulu ili kulinda heshima
yako kama msomi Professor, pia kulinda heshima serikali na Chama
tawala. Huwezi kutumikia ofisi mbili, yaani utumishi wa umma na
biashara.
Wanachi
tunasikitika sana kuona katika sakata la fedha za umma mpaka baadhi
watumishi wa Mungu ambao ni viongozi wa Kanisa nao wanahusika na bila
ya woga. Wanapokea fedha bila ya hofu ya kujenga udini.