Hesabu mpya kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Ebola iliyotolewa na shirika la afya duniani WHO inaonyesha kuwa karibu watu 7000 wameaga duian kutokana na ugonjwa wa Ebola wengi wakiwa eneo la Afrika magharibi.
Hili
ni ongezeko la zaidi ya watu 1000 tangu WHO itoe hesabu yake ya
mwisho siku nne zilizopita.
Sehemu
kubwa ya ongezeko hilo iliripotiwa nchini Liberia
Mkuu
wa ujumbe wa umoja wa mataifa unaohusika na ugonjwa wa Ebola Antony
Banburry anasema kuwa kwa sasa nchi iliyoathirika zaid ni Sierra
Leone ambapo karibu visa 500 vya ugonjwa wa Ebola huripotiwa kila
wiki.
Amesema
kuwa maziko ambayo ndiyo chanzo kikubwa cha maambukizi bado
hayafanywi kwa njia iliyo salama.
0 comments:
Post a Comment