Wednesday, 10 December 2014

Kilio cha Albino Tanzania...


Mtobi Namigambo, ni mvuvi anayeuza samaki, amekaa kwa utulivi nje ya nyumba yake ya matope katika kisiwa cha ukerewa mahali ambapo zamani palikuwa makao ya albino lakini kwa sasa si hivyo. Mtoto wake wa miaka nne May Mosi ameketi kwenye paja lake akionyesha umarufu wake wa hisabati kwa kuhesabau moja hadi kumi kwa ujasiri.
Mara kwa mara Mtobi anamtazama mke wake, Sabina, ambaye ameketi kwa mkeka kando yake akitayarisha chakula cha jioni. Watoto wake wengine wawili wanachezea hapa karibu na pia wamejaliwa na mtoto mchanga amabye yuko chumbani analala.
May alipokuwa na umri wa miezi mitatu, aliponea jaribio la kutekwa nyara.
" nilikuwa nimeenda ziwani kuvua samaki. walikuwa pekee yao nyumbani wavamizi walipokuja, mke wangu alitorokea kwa dirisha na kukimbillia usalama akiwa na May, na akawawacha watoto hawa wawili nyumabani ambao hawakuwadhuru kabisa", Mtobi ananiarifu.
"Wavamazi hao walikuwa wakimtaka May," Sabina anaongezea, "mume wangu alikuwa ameenda safari ya uvuvi na wavamizi hao walijua na hio ndio sababu walikujia mtoto wangu, baada ya kutorokea kwa dirisha, bado waliniandama huku nikipiga mayoye ya usaidizi, waliwacha kuniandama wakati tu niliwaamsha majirani"
May ni mojawapo wa Albino sabini wanaoishi katika kisiwa hiki cha Ukerewa ambacho ni masaa matatu tu kutoka mwanza, mji wa pili mkubwa zaidi Tanzania.
Elimu kwa jamii
Mtobi anasema "tunaiomba serikali kufanya juhudu zaidi za kuelimisha jamii hapa, serikali ishawahi kuandaa majadiliano kuhusu Albino na kulikuwa na mabadiliko makuwa, akini si hivyo tena"
Shirika lisilo la kiserekali chini ya mrengo wa 'The Same Sun' linalowashughulikia jamii ya Albino hapa Ukerewa, linasema kuwa kisiwa hiki hakina usalama kando na vile watu wangependa kuamini.
Mwenye kiti wa chama cha maalbino tawi la Mwanza, (TAS) Alfred Kapole, mzaliwa wa Ukerewe, alilazimika kutorokea mji wa Mwanza akiwa mmoja wa albino wa kwanza kufika kortini baada ya kiognozi mmoja wa kijiji akitaka kumuua kwa ajili ya nywele zake.
Mwaka uliopita boma lake lilivamiwa, kwa bahati nzuri alikuwa ameenda mwanza. Kulikuwa na jairibio lEngine la kumuua mwaka huu.
Kampeni kabambe
Serikali ya Tanzania imeanzisha kampeni ili kuchangisha fedha za kuelimisha jamii.
Kampeni nyingi za uhamasishaji hufanyika mijini kwani ni rahisi kufikia watu,lakini ni vijiji ndivyo vinahitaji msaada zaidi.
Ramadhan Khalfan, ambaye ni mwenyekiti wa chama cha albino Ukerewa,anasema kuwa wanataka kufikia maeneo ya vijiji na kuzungumza na watu,lakini ni vigumu kutokana na ukosefu wa fedha za kutosha.''Hatuna uwezo ama njia za kufikia jamii zilizoko vijijini.Aliongezea kusema,''tunategemea pakubwa redio na televisheni,lakini hatuwezi kufika mashinani kwa sababu ya gharama.''
Sehemu ya Serengema inapatikana kilomita 60 (maili 33.5) kutoka Mwanza.Ili kusisitiza shida hii,umejengwa mnara katika mzunguko katikati ya mji.
Ni sanamu ya chuma kimo cha binadamu,inayoonyesha baba mwenye rangi akimbeba begani mto wake albino huku mama yake mwenye rangi akitundika kofia yenye ukingo mpana kwenye kichwa cha mwana huyo kumkinga kutokana na miale ya jua.Pia kuna majina ya watu 139 ya waathiriwa waliouawa,kuvamiwa ama miili yao kuibiwa kutoka kwenye makaburi.
Serengema ndio sehemu iliyoathirika vibaya zaidi.
Kuna mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi pamoja na chama cha Tanzania Albino katika kuhamasisha na pia kujenga makaazi.
Mashirika yasiyo ya kiserikali yanaamini kuwa uhamasisho na kuacha imani potovu zinaweza kusimamisha mauaji haya.
Mwakilishi wa chama cha Serengema Mashaka Benedict anasema kuwa watu bado wanaamini kuwa sehemu za mwili wa albino zinaweza kuleta utajiri.''Kama hiyo ndiyo hali,mbona sisi si matajiri?''anauliza.
Anadai kuwa watu mashuhuri wanahusika katika ''biashara ya mauaji'' na ndio maanake watu wachache sana wamekamatwa,kushitakiwa,kupatikana na hatia ama kufungwa.''Itakuwa vipi masikini kutoa dola 10,000 kwa kipande cha mwili?,ni wanabiashara na wanasiasa ndio wanaohusika.''
Hata hivyo polisi wanasema kuwa wanachungunza kila moja ya visa lakini wanakosa ushahidi wa kuthibitisha madai yanayotolewa.Kamanda wa polisi wa Mwanza,Valentino Mlolowa anasema,''Kesi hizi ni ngumu kwa kuwa visa hufanyika mashinani sana katika sehemu ambazo hazina stima kwa mfano,na hiyo inafanya kuwajua wahalifu usiku kuwa vigumu.Tunachunguza kila moja ya kesi na madai,lakini kama uonavyo,si rahisi.''
Yaweza onekana kama kuwa tumepoteza kila kitu lakini hii haiwazuilii watu wanaoishi na hali ya Uhalbino kama May Mosi,kutokuwa na tumaini kuwa fedha zinazochangishwa kutoka kwenye kampeni iliyoanzishwa na serikali zitasaidia kusikizwa zaidi kwa Albino nchini Tanzania.





Share:

0 comments:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.