Tuesday, 16 December 2014
Home »
» ''Niliokoa Kenya 2013'' asema Moreno Ocampo.
''Niliokoa Kenya 2013'' asema Moreno Ocampo.
Kiongozi wa zamani wa mashitaka katika mahakama ya jinai ya ICC, ameteta uamuzi wake wa kumshitaki Rais Uhuru Kenyatta licha ya kesi hiyo kutupiliwa mbali.
Bwana Luis Moreno Ocampo anasema kua mashitaka hayo dhidi ya Uhuru yalizuia ghasia kutokea tena katika uchaguzi wa mwaka 2013.
Kenyatta alishinda uchaguzi huo baada ya kugombea kwa tiketi ya chama cha TNA, huku akiituhumu mahakama hiyo kwa kuingilia maswala ya ndani ya Kenya.
Alishtakiwa kwa kosa la kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007.
Wiki jana mrithi wa Ocampo, Fatou Bensouda, alitupilia mbali kesi hio dhidi ya Kenyatta akisema amekosa kupata ushahidi wa kutosha kuthibitisha mashitaka dhidi ya Uhuru.
Kenyatta hata hivyo tangu mwanzoni alikanusha madai ya kutenda uhalifu dhidi ya Binadamu.
Alikuwa Rais wa kwanza aliye mamlakani kuwahi kufikishwa katika mahakama hio ambayo wengi wanasema ni ya kisiasa.
Watu 1,200 walifariki na wengine 600,000 kutoroka makwao katika ghasia hizo ambazo ndio mbaya zaidi kuwahi kushuhdiwa nchini humo tangu ijinyakulie uhuru.
Ocampo aliambia BBC kwamba kushitakiwa kwa Uhuru kulizuia ghasia kutokea tena nchini Kenya, wakati wa uchaguzi mwaka 2013. ''Mahakama ya ICC ilibadilisha siasa za Kenya, '' alisema Ocampo.
Wiki jana Rais was Uganda Yoweri Museveni alirejelea wito wake kwa mataifa ya Afrika kujiondoa ICC akisema kuwa mahakama hio inakandamiza mataifa ya Afrika.
Hata hivyo Ocampo amesema mahakama ya ICC ilikuwa kizingiti kwa viongozi kumi ambao walitegemea na kutumia sana ghasia ili kusalia mamlakani.
0 comments:
Post a Comment