Saturday, 25 April 2015
Home »
» Mwanaharakati maarufu auawa Pakistan
Mwanaharakati maarufu auawa Pakistan
Mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu nchini Pakistan Sabeen Mehmud ameuawa kwa kupigwa risasi kwenye mji mkuu Karachi.
Alivamiwa na watu wasiojulikana alipokuwa akielekea nyumbani kwake baada ya kuandaa warsha kuhusu kuhusika kwa jeshi la Pakistan katika kuwatesa na kuwaua wanaharakati wa kisiasa nchini humo.
Bi Sabeen ambaye alikuwa na umri wa miaka 38, alikuwa pia mkurugenzi wa shirika moja la misaada na wa duka moja la vitabu ambapo mazungumzo kuhusu haki za binadamu yalikuwa yakifanyika.
Duka hilo lilikuwa moja ya maeneo machache mjini Karachi ambapo wanafunzi na wanaharakati walikuwa wakikutana kujadili changoto zinazoikumba Pakistan.
0 comments:
Post a Comment