Wednesday, 15 July 2015

Wairan wafurahia makubaliano ya nyuklia.


Maelfu ya raia wa Iran wamekuwa wakishangilia mitaani kufutia makubaliano mapya ya mpango wa nyuklia kati ya Iran na mataifa makubwa yenye nguvu dunian ambapo sasa Iran itapunguziwa vikwazo vya kiuchumi.
Hata hivyo katika makubaliano hayo Iran imepewa masharti katika harakati zake za kutengeza nuklia.
Huenda hatua ya kupunguziwa vikwazo vya kiuchumi vikawa vimechangia furaha ya wa Iran wengi katika makubaliano hayo ambapo Kiongozi mkuu wa Kidini Ayatollah Ali Khamenei alipongeza juhudi za wapatanishi kutoka Iran.
Hata hivyo kumekuwa na hisia tofauti kwa mataifa ya kiarabu na yale ya mashariki ya kati kufuatia makubaliano hayo ya nyuklia ya Irani.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu amepinga kwa nguvu zote mapendekezo ya makubaliano hayo yaliyofikiwa. Ambapo katika makubaliano hayo Iran itaondolewa vikwazo vya kiuchumi vya kimataifa, kwa Iran kuacha kutengeneza silaha za nyuklia.
"Bila kugawanya mpango huu wa nyuklia wa Iran, katika miongo, mpango huu hautabadili chochote, hautawafanya Iran wajutie makosa yao, na unajenga utawala wa kigaidi kwa kuwa na uwezo wa kutengeneza mabomu ya nyuklia, ki ukweli silaha zote za nyuklia na namna ya kuziendeleza. Kosa hili kubwa ni la kushtua na kushangaza. Israel haitahusika na makubaliano hayo na Iran, kwa sababu Iran imekuwa ikifanya mipango ya kutuharibu. Tutaendelea kujihami wenyewe." Amesema Netanyahu.
Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje wa Iran ameiambia BBC makubaliano hayo ya nyuklia ni hatua mojawapo ya kuimarisha uhusiano kati ya Iran na mataifa ya magharibi. Amesema ushirikiano mkubwa unahitajia kupambana na vitisho vya Islamic State.
Share:

0 comments:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.