Ripoti
kutoka kaskazini-mashariki mwa Nigeria zinaarifu kuwa kundi la
wapiganaji Waislamu la Boko Haram, limefanya mashambulio mawili
makubwa katika siku chache za karibuni ambapo watu karibu 100
wameuwawa.
Kiongozi
mmoja katika jimbo la Borno alisema kuwa wapiganaji waliuwa wauza
samaki karibu 50 karibu na kijiji cha Doron Baga, kando ya Ziwa Chad.
Alisema
wapiganaji wa Boko Haram wameweka kizuizi kwenye njia ya kuelekea
Chad na kuwakamata wachuuzi waliokuwa wakienda kununua samaki.
Katika
tukio jengine hapo awali watu karibu 50 waliripotiwa kuwa waliuwawa
karibu na mpaka wa Cameroon pale Boko Haram walipovamia kijiji cha
Azara Kuya, siku ambapo soko huwa na watu wengi
0 comments:
Post a Comment