Watu
kumi wamepoteza maisha baada ya jengo la ghorofa kuanguka mjini Cairo
nchini Misri, maafisa wameeleza.
Watu
saba wamejeruhiwa baada ya jengo la ghorofa nane kuanguka usiku.
Mkuu
wa Idara ya dharula Jenerali Mamdouh Abdul Qader amesema vikosi vya
uaokoaji vinawasaka Watu 15 wanaokisiwa kunasa kwenye kifusi.
Mara
kadhaa majengo yameanguka nchini humo, sababu kubwa ikiwa ujenzi
usiofuata kanuni na Sheria pia usimamizi mbovu wa taratibu za ujenzi.
Jenerali
Qader ameliambia shirika la Habari la Ufaransa kuwa hawajui chanzo
cha ajali hiyo,lakini walipatiwa taarifa kuwa ghorofa mbili za juu
zilijengwa kinyume cha sheria.
Wakazi
wa majengo ya karibu na lilipoanguka jengo hilo wameondoka katika
makazi yao kwa nia ya kujihadhari.
Mwezi
Januari Mwaka jana,Watu 28 walipoteza maisha baada ya jengo la
ghorofa nane kuanguka mjini Alexandria.
0 comments:
Post a Comment