Ikulu
ya white house nchini Marekani inasema kuwa rais Barack Obama amemteua
mwendesha mashtaka wa mji wa New York Loretta Lynch kuwa mkuu wa
sheria nchini humo. Msemaji
wa ikulu ya white house alisema kuwa mkuu huyo mpya wa sheria
atateuliwa rasmi leo Jumamosi. Ikiwa
uteuzi wake utaidhinishwa na bunge la seneti Loretta Lynch atakuwa
mwanamke wa kwanza mwenye asili ya afrika kuwa mkuu wa sheria nchini
marekani . Uteuzi
huo unafanyika wiki sita baada ya kujiuzulu kwa Eric Holder ambaye
ndiye M'marekani wa kwanza mweusi kuteuliwa kuwa mkuu wa sheria
nchini humo.
Saturday, 8 November 2014
Home »
» USA:Mwanamke mweusi (Loretta Lynch)ateuliwa kuwa mwanasheria mkuu wa marekani...... BBC
0 comments:
Post a Comment